• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Wasiwasi waibuka Embu watu 15 wakijitoa uhai ndani ya miezi mitatu

Wasiwasi waibuka Embu watu 15 wakijitoa uhai ndani ya miezi mitatu

NA GEORGE MUNENE

KAMISHNA wa Kaunti ya Embu Jack Obuo ameelezea wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa watu wanaojitoa uhai baada ya visa 15 kurekodiwa katika kaunti hiyo ndani ya miezi mitatu.

Amefichua kuwa watu watano walijitia kitanzi mnamo Septemba, wanne Oktoba na sita Novemba, hali inayoashiria mtindo wa watu kujitoa uhai akisema inahofisha.

Akizungumza katika kikao cha usalama kilichofanyika afisini mwake, afisa huyo alisema wahasiriwa wote ni wanaume jambo linaloweza kuhusishwa na hali ya wanaume kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha.

Katika visa vyote, alisema hakukuwa na barua yoyote iliyoachwa na wahasiriwa huku wengi wao wakijinyonga.

Alisema idadi kubwa ya visa hivyo vimefanyika katika maeneo ya Embu Mashariki na Magharibi yanayohusishwa na visa vingi vya mafarakano ya kifamilia na matatizo kiuchumi.

Bw Obuor ametoa wito kwa jamii kuwa makini na kuwasaidia walio na matatizo ili kupunguza visa hivyo kwa sababu wengi wao huishia kujiua kwa kukosa kusaidiwa kihisia na kisaikolojia.

Wakati huo vilevile, ametangaza msako mkali kuhusu pombe haramu na mihadarati ambazo pia zimechangia kuongezeka kwa visa vya watu kujitoa uhai na uhalifu.

Alisema tayari wamewatambua wanaohusika na biashara hiyo haramu na watakabiliwa kisheria hivi karibuni.

Ameonya kuwa wanaohusika na uundaji wa pombe haramu hawataepuka mkono wa sheria.

Msimamizi huyo amesema serikali imejitolea kuhakikisha pombe haramu zimezimwa.

  • Tags

You can share this post!

Bobi Wine ashambuliwa kwa madai yake kuhusu sheria ya...

Arsenal wataruka kamba ya Aston Villa ugani Villa Park?

T L