• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:50 AM
Watu 26 wafariki kwa corona

Watu 26 wafariki kwa corona

Na CHARLES WASONGA

WATU 26 zaidi wamethibitishwa kufariki kutokana na Covid-19 jana Alhamisi huku watu wengine 1,463 wakiambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Visa hivyo vipya vimegunduliwa baada ya sampuli 8,976 kupimwa na hivyo kuandikisha kiwango cha maambukizi cha asilimia 16.3.

Miongoni mwa watu hao wapya waliopatikana na virusi vya corona, 1,428 ni Wakenya ilhali 35 ni wageni. 802 katika ni wanaume huku 661 wakiwa wanawake.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Alhamisi na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, jumla ya wagonjwa 498 walithibitishwa kupona ndani ya saa 24 zilizopita. 372 walikuwa wakiuguzwa nyumbani ilhali 126 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali.

“Kwa hivyo jumla ya wagonjwa 91,268 wamepona tangu ugonjwa huo uliporipotiwa nchini Machi 2020,” ikasema ripoti hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa jumla ya wagonjwa 1,080 wa corona wakati huu wamelawa katika hospitali mbali mbali nchini huku 3,825 wakihudumiwa nyumbani.

“Wagonjwa 121 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 35 miongoni mwao wakisaidiwa kupumua kwa mitambo ya ventilators. Wengine 77 wanaongeza hewa ya oksijeni kwa njia za kawaida

Kwa misingi ya kaunti, Nairobi inaongoza kwa kuandikisha visa vipya 766 vya maambukizi ya corona.

Nakuru inafuatia kwa visa 126, Meru 83, Uasin Gishu 74, Kiambu 49, Kitui 46, Machakos 44, Kericho 30, Kisumu 28, Mombasa 27, Kajiado 22, Migori 20, Bungoma 20, Busia 19, Narok 17, Nyamira 16, Kilifi 15, Laikipia 11, Bomet 9, Garissa 7, Siaya 7, Nandi 5, Nyeri 5, Kisii 3, Elgeyo Marakwet 2, Kirinyaga 2, Makueni 2 na Trans Nzoia 2.

Nazo kaunti za Nyandarua, Tharaka Nithi, Vihiga, Kwale, Baringo, na Wajir zimeandikisha kisa kimoja kila moja.

  • Tags

You can share this post!

Harambee Stars nje ya safari ya kufika Cameroon kwa AFCON...

AKILIMALI: Jinsi unavyoweza kuzalisha mparachichi kutoka...