• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 12:05 PM
Wito akina mama wafanye biashara ili kujikimu

Wito akina mama wafanye biashara ili kujikimu

Na WINNIE ATIENO

MBUNGE wa Nyali Bw Mohammed Ali na Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Mombasa, Bi Zamzam Mohammed wamewasihi wanawake katika eneo hilo kujishughulisha na biashara ili kujikimu.

Wakizungumza kwenye hafla ya kuwapa wanawake wa makundi 70, Sh5.2 milioni za kuwawezesha kiuchumi katika uwanja wa shule ya msingi ya Khadija, walisema wataendelea kuwasaidia akina mama ili wajikwamue kiuchumi.

“Wanawake ndio wanaosimamia jamii tutaendelea na miradi ya kuwapiga jeki,” akasema Bw Ali Bi Mohammed aliwasihi wanawake kukumbatia maendeleo.

“Tumieni fedha hizo kujiimarisha na kuinua uchumi wa Mombasa kupitia biashara,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti yatoa ilani kuzika miili

Raia wa kigeni ‘anayeuza’ watu afurushwa

T L