• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
6 waotea kiti cha Ojaamong

6 waotea kiti cha Ojaamong

SHABAN MAKOKHA na SAMWEL OWINO

WAWANIAJI sita wametangaza azma yao ya kuchukua usukani wa Kaunti ya Busia kutoka kwa Gavana anayeondoka Sospeter Ojaamong katika Uchaguzi Mkuu 2022.

Bw Ojaamong’ ataondoka afisini baada ya kuapishwa kwa mrithi wake akiwa amehudumu hatamu mbili kikatiba tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kama Gavana wa kwanza 2013.

Miongoni mwa wanaomezea mate kumrithi ni mbunge wa zamani wa Amagoro pamoja na naibu wake Moses Mulomi, mbunge wa zamani Funyula, Paul Otuoma, Mwakilishi Mwanamke katika Kaunti Florence Mutua, Mbunge wa Nambale John Bunyasi, Mkurugenzi wa Mamlaka inayosimamia bandari Nchini (KPA) Vincent Sidai na aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri inayosimamia Fedha za Kilimo Lucas Meso.

Bw Otuoma aliwania kiti hicho 2017 lakini akashindwa na Bw Ojaamong baada ya kutema chama cha ODM na kuwania kama mgombea huru akidai maafisa kutoka Orange House walikuwa wamemwibia kura Bw Ojaamong.

Anatarajiwa tena kumenyana na Bi Florence Mutua, anayejivunia uhusiano wa karibu kisiasa na Kiongozi wa ODM Raila Odinga wakati wa teuzi za ODM katika juhudi zake za kupeperusha bendera ya chama huku akijaribu kuwania kwa mara ya pili afisi ya ugavana.

Bw Otuoma, ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Ubinafsishaji amesema atafanya kila awezalo akidai ana uwezo wa kuongoza Busia katika hatua nyingine kimaendeleo na kuboresha maisha ya wakazi.Naibu Gavana Moses Mulomi amesalia mstari wa mbele na sauti kuu katika kumwakilisha Gavana kwenye hafla kaunti hiyo katika juhudi za kupata uongozi wa kaunti.

Anatarajia uhusiano wa karibu wa kufanya kazi kati yake na Bw Ojaamong utamfanya kiongozi bora.“Uhusiano wangu wa karibu na Gavana umenipa fursa ya kujifunza jinsi shughuli za kaunti zinavyoendeshwa. Alisema Bw Mulomi.

You can share this post!

Hoki: Vipusa wa kitaifa waanza Jamhuri Cup kwa madaha

Naibu Chansela hatarini kufungwa kwa kukaidi korti

T L