• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 3:19 PM
Gavana Mung’aro apendekeza Mackenzie afungwe maisha

Gavana Mung’aro apendekeza Mackenzie afungwe maisha

Na ALEX KALAMA 

HATIMAYE Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro amevunja kimya chake kuhusu mchungaji tata wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie anayeaminika kushawishi watu kufunga hadi kufa kwa kisingizio cha kukutana na Yesu.

Akitoa kauli yake kuhusu madai yanayozingira mhubiri huyo, Bw Mung’aro amesema sababu moja ambayo mahakama imekuwa ikimuachilia Mackenzie mara si moja kila anapofikishwa katika mahakama kuu ya mji wa Malindi, ni kwamba Ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka unakosekana.

“Mackenzie ameshikwa mara nyingi na kuachiliwa, sababu moja ya korti ambayo wametupatia ya yeye kuachiliwa ni kwamba hakukuwa na ushahidi wa kuonyesha kuwa watu wamekufa kwa ajili ya njaa,” alisema.

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro. Picha / ALEX KALAMA

Watu wanne wamethibitishwa kufa njaa, kufuatia hadaa za mchungaji huyo.

Alisema kwa sasa mtaalamu wa upasuaji wa maiti katika Hospitali Kuu ya Malindi yuko likizo, lakini ametakiwa kurejea kazini kabla likizo yake kukamilika ili kufanyia upasuaji miili hiyo.

Kulingana na gavana, ni kwamba kama kaunti wamejipanga na wameweka mikakati ya kutosha kuhakikisha kwamba miili ya wafuasi hao wa Mackenzie wanaodaiwa kufariki kwa kutokula wala kunywa maji kwa muda mrefu baada ya kushawishika na mafunzo potovu itafanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu juma lijalo.

Mung’aro alisema iwapo ukweli utabainika kwamba walikufa kwa sababu ya njaa, basi serikali ya Kaunti ya Kilifi itahakikisha Mackenzie anachukuliwa hatua kali kisheria ikiwemo kufungwa maisha.

“Ikibainika walikufa kwa sababu ya njaa, tutahakikisha mchungaji Mackenzie anafungwa maisha kwa sababu amepoteza maisha ya watu wengi,” aliahidi gavana.

  • Tags

You can share this post!

Kondoo 50 walioibwa shamba la Kenyatta warejeshwa 

MAPISHI KIKWETU: Viazi vitamu vilivyookwa...

T L