• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 1:22 PM
Watupwa jela miaka 7 kwa kunaswa na jino la kiboko

Watupwa jela miaka 7 kwa kunaswa na jino la kiboko

Na BRIAN OCHARO
NDUGU wawili wamefungwa jela miaka saba baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki kiharamu jino la kiboko lenye uzito wa kilo 1.9 na thamani ya Sh50, 000.

Hakimu wa Mahakama ya Shanzu, Bw David Odhiambo, alisema kulikuwa na ushahidi wa kutosha uliowasilishwa dhidi ya washtakiwa Joseph Molel na Joshua Molel.
Mahakama iliambiwa kuwa, makosa hayo yalitendwa mnamo Julai 29, 2021 huko Mtwapa, Kaunti ya Kilifi.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Nadrat Mazrui uliwasilisha mashahidi wanne.
Wawili hao walishtakiwa pia kwa kuhusika na biashara haramu ya wanyamapori bila kibali.

  • Tags

You can share this post!

MAADHIMISHO: LEBA DEI 2023

Wahubiri North Rift: Tuko tayari kupigwa msasa

T L