• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Asante Mlima Kenya kwa kukataa kuwa mateka wa Uhuru Kenyatta, Ruto ashukuru

Asante Mlima Kenya kwa kukataa kuwa mateka wa Uhuru Kenyatta, Ruto ashukuru

NA MWANGI MUIRURI

RAIS William Ruto Jumapili, Agosti 6, 2023 akiwa katika Ikulu ndogo ya Sagana, Nyeri aliwashukuru wapiga kura wa Mlimani kwa kukaidi Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliyekuwa akiwaelekeza wamuunge mkoono Raila Odinga.

Bw Kenyatta alikuwa amezindua njama kali ya kumzuia Naibu wake, Bw Ruto, kurithi urais, akipendelea Bw Odinga ambaye alikuwa mpinzani wake mkuu katika chaguzi za 2013 na 2017.

Odinga alikuwa amesababisha kufutiliwa mbali kwa ushindi wake wa 2017 na mahakama ya upeo na ukarudiwa na akashinda tena baada ya mpinzani huyo kususia kura ya marudio.

Dkt Ruto alisema kwamba kwa kususia kauli ya Bw Kenyatta, wapiga kura wa Mlimani walidhihirisha uungwana na ustaarabu.

Aidha, alisema hatawaangusha katika kuwatuza maendeleo.

“Kwa mfano, hawa madalali wa kahawa, majanichai na maziwa yasiwahangaishe. Mimi ndiye nitawakomoa mpaka watii. Hali itakuwa sawa na pato litaongezeka,” akasema.

Alisema kwamba hakuna maziwa ya unga itaingizwa hapa nchini kutoka taifa jirani la Uganda, maziwa hayo yakihusishwa na familia moja kuu ya Mlimani.

Aidha, alisema kahawa ya wakulima ambayo ilikuwa imekwama katika hifadhi kufuatia hatua ya serikali ya kuondoa leseni za madalali sasa itapata soko.

Alisema kahawa hiyo itauzwa mwezi ujao, Septemba huku mbunge wa Githunguri Bi Gathoni wa Muchomba akipendekeza serikali kwanza itoe pesa za kununua kahawa hiyo ikingoja soko hilo.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Lalama utatuzi masuala ya Tsavo unakawia

Ruto: Ukusanyaji ushuru ndio utanusuru Kenya, tukaze mshipi...

T L