• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:36 PM
Kenya yazindua setlaiti ya kwanza kusaidia kuboresha kilimo na mazingira

Kenya yazindua setlaiti ya kwanza kusaidia kuboresha kilimo na mazingira

Na WINNIE ONYANDO

SERIKALI ya Kenya imezindua setlaiti ya kwanza Taifa -1, iliyogharimu Sh50 milioni.

Katibu katika Wizara ya Ulinzi, Patrick Mariru, alisema setlaiti hiyo ilisanikishwa na wahandisi wa ndani kutoka Shirika la Anga la Kenya.

“Ni jambo la kusherehekea Kenya kuzindua setlaiti itakayotumika kuangazia masuala mbalimbali. Japo hatukupata wahandisi kutoka nje ya nchi, wahandisi wetu wa ndani waliweza kuunda kila kitu.”

“Gharama imekuwa ya kawaida. Kutengeneza setlaiti hiyo iligharimu Sh50 milioni,” akasema Bw Mariru.

Hata hivyo, afisa huyo alibainisha kuwa uzinduzi huo utategemea hali ya hewa, miongoni mwa hali nyingine.

Uzinduzi huo, ambao umepangwa kusaidiwa na Space Exploration Technologies Corporation (SpaceX), utafanyika Vandenberg Base, California, UDA aboard Falcon-9 Rocket.

Setlaiti itatoa data kwa ajili ya usaidizi wa maamuzi kwa kilimo na usalama wa chakula, usimamizi wa maliasili na ufuatiliaji wa mazingira miongoni mwa maelezo mengine.

“Tunalenga kusaidia serikali yetu kufanya maamuzi kwa kuzingatia takwimu kwa mfano upandaji miti au mabadiliko ya tabia nchi. Sasa tuna chombo chetu cha kukusanya takwimu, hatuhitaji kwenda kwa mashirika mengine nje ya nchi kuchukua data,” akaongeza Bw Mariru.

  • Tags

You can share this post!

KINYUA KING’ORI: Maridhiano baina ya Rais Ruto na...

Adan Mohamed na Ahmed Kolosh wapewa mnofu serikalini

T L