• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 12:25 PM
Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini- NSDCC

Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini- NSDCC

NA LEON LIDIGU

Maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini yamepungua kutoka 34,540 hadi 22,154 mwaka 2022, kulingana na matokeo ya hivi karibuni ya Baraza la Taifa la Kudhibiti Magonjwa ya Magonjwa nyemelezi (NSDCC).

Kulingana na ripoti yao ya mwaka 2022, takwimu rasmi zinaonyesha kuwa idadi ya watu wanaoishi na virusi hivyo ilipungua kutoka milioni 1.4 mwaka jana hadi milioni 1.37 mwaka huu.

“Idadi ya vifo ilipungua kutoka 22,373 hadi 18,473 huku maambukizi ya ukimwi kwa wanawake yakiwa asilimia 5.3 na wanaume asilimia 2.6,” Mkurugenzi Mtendaji wa NSDCC Dkt Ruth Laibon-Masha aliambia Taifa Leo katika mahojiano, huku akiangazia kwamba idadi ya Wakenya wanaopata matibabu ya kurefusha maisha iliongezeka kutoka milioni 1.12 hadi milioni 1.29.

Kulingana na matokeo mapya, maeneo ya Nyanza, Magharibi na Pwani yanaendelea kuongoza kwa idadi ya watu walioambukizwa Ukimwi.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wapata afueni kwenye kesi ya mauaji

Korti yaita maafisa 2 wa polisi kujibu madai ya kukarabati...

T L