• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Mahakama Kuu yaonya jopo la uchunguzi Shakahola

Mahakama Kuu yaonya jopo la uchunguzi Shakahola

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imeyumbisha tume iliyoteuliwa na Rais William Ruto kuchunguza mauaji ya mamia ya waumini katika msitu wa shakahola.

Jaji Lawrence Mugambi aliiamuru isithubutu kuanza shughuli zake hadi atoe mwelekeo.

Kinara wa Azimio Raila Odinga alishtaki serikali akisema Rais Ruto amekaidi Katiba na kutwaa mamlaka yasiyo yake alipoteua jopo hilo.

Jaji Mugambi alisitisha kazi ya jopo hilo linaloongozwa na Jaji Jessie Lesiit wa Mahakama ya Rufaa.

Aidha, Jaji huyo alitoa agizo hilo kufuatia kesi iliyoshtakiwa na Chama cha Azimio kupitia wakili Paul Mwangi.

Katika mawasilisho yake mbele ya Jaji Mugambi, Bw Mwangi alisema Rais Ruto alijitwalia mamlaka ambayo hajakabidhiwa kisheria kuteua jopo la kuchunguza kanisa la Pasta Paul Mackenzie.

Mbali na shughuli za kanisa hilo la Mackenzie, jopo hilo litachunguza shughuli za makanisa ambayo yanatoa mafundisho ya kupotosha.

Azimio katika kesi hiyo imesema kuwa Rais Ruto aliteua jopo hilo ilhali kuna asasi nyingine zinazochunguza mauaji ya Shakahola.

“Kuna kamati ya seneti inayoongozwa na Seneta wa Tana River Danson Muungatana,” alisema Bw Mwangi.

Pia alisema polisi wanaendelea kuchunguza Mackenzie.

Mackenzie anazuiliwa kuchunguzwa kwa mauaji ya haliaiki ya watu, mafundisho yenye itikadi kali ambapo wafuasi wanatakiwa kufunga hadi kufa ndipo wamwone Yesu.

Bw Mwangi amemkosoa Rais Ruto akisema ametwaa majukumu ya bunge, mashirika huru kutetea haki za binadamu nchini, mamlaka huru ya polisi (IPOA) na tume ya huduma za mahakama (JSC).

Wakili huyo pia alisema Rais Ruto alinyakua mamlaka ya Jaji Mkuu Martha Koome, ambaye angemsaidia katika uteuzi huo.

Akipinga kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu kupitia kwa wakili wa serikali Emmanuel Mbita, alimtetea Rais Ruto akisema hajakaidi sheria na Katiba.

“Rais Ruto amejukumika kisheria kutetea haki za kila mwananchi,” Bw Mbita.

  • Tags

You can share this post!

Kioni, Murathe warudishwa katika uongozi wa Jubilee

Mkurugenzi wa Kebs mashakani kwa wizi wa sukari hatari

T L