• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 2:32 PM
Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa DCI naye auawa kwa risasi

Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa DCI naye auawa kwa risasi

NA MWANGI MUIRURI

IDARA ya polisi Jumanne imefichua kwamba imemuua kwa kumpiga risasi mshukiwa wa ujambazi, John Kamau almaarufu Johnte au Farouk, ambaye inadaiwa alimuua afisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) David Mayaka mnamo Agosti 8, 2023 mtaani Kayole.

Mnamo Agosti 22, 2023 Bw Wambugu amesema kwamba mshukiwa huyo katika mauaji hayo ya Bw Mayaka alifuatwa hadi kwenye makao yake katika mtaa wa Ruai na baada ya kutangaziwa alikuwa na wageni kutoka DCI na kutakiwa ajisalimishe, aliwakaribisha kwa kuwafyatulia risasi.

“Nao maafisa walijibu makaribisho hayo kwa risasi na hali ikaishia kuuawa kwa Kamau almaarufu Johnte au Farouk. Afisa mmoja amepata jeraha kwa paja na amepelekwa hospitalini,” akasema Bw Wambugu.

Bunduki aina ya CZ ikiwa na risasi 12 imepatikana kutoka kwa mshukiwa huyo na pia simu kadha zinazoshukiwa kuwa za kuibiwa.

Afisa huyo alikuwa ameharibikiwa na gari lake akiandamana na mke wake na akiwa katika harakati za kulirekebisha, wakavamiwa na genge la watu watatu waliokuwa wameabiri pikipiki na ambapo alipigwa risasi na kuuawa.

Mke wa afisa huyo alipigwa risasi mguuni na akakimbizwa hospitalini kutibiwa.

Afisa huyo naye aliaga dunia.

Mnamo Agosti 16, 2023 maafisa wenzake wakiwa katika msako mkali wa genge hilo walimtia mbaroni mmoja wa washukiwa hao watatu.

Kamanda wa Polisi wa Kayole Bw Paul Wambugu aliambia Taifa Leo kwamba mshukiwa huyo kwa jina Alex Wanjiru mwenye umri wa miaka 23 alinaswa katika boma moja la Kaunti ya Kiambu akiwa amejificha ndani ya chumba cha malazi cha nyanyake. Bw Wambugu alifichua wakati huo kwamba pikipiki iliyotumika katika kisa hicho ilikuwa imenaswa ikiwa ni muundo wa Boxer yenye usajili KMGJ 350V.

Bw Wambugu amesema kwa sasa anayewindwa ni mshukiwa mwingine kwa jina Henry Njihia ambaye alikuwa wa tatu katika kisa hicho cha mauaji ya Bw Mayaka.

“Hata yeye taarifa hii impate popote alipo ajue kwamba tuko mbioni kumnasa. Ninamshauri ajisalimisha lakini uamuzi ni wake,” akasema Bw Wambugu.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Nyota 5 kuwakilisha Kenya kwenye Mashindano ya Dunia ya...

KRA yapata Kamishna Mkuu mpya

T L