• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Uhuru aapa kuwa BBI itatimia

Uhuru aapa kuwa BBI itatimia

Na CHARLES WASONGA

KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa Maridhiano (BBI) sharti yatatekelezwa.

Akiongea Jumapili katika bustani ya Jamhuri, jijini Nairobi, wakati wa sherehe za 57 za Jamhuri Rais alisema kuwa mchakato huo utachangia kupililia umoja ambao mashujaa wa uhuru walipigania tangu 1963.

“Tunahitaji kuziba nyufa katika ukuta wa taifa letu kulinga na ndoto ya waanzilishi wa taifa hili. Na hii itawezekana tu endapo tutakomesha uchaguzi wa mshindi anatwaa kila kitu. Hii lengo ambalo BBI ililenga kutimiza na ninaamini litatimia licha ya vizingiti vilivyowekwa na mahakama,” Rais Kenyatta akasema.

“BBI ni ndoto iliyoahirishwa tu. Siku moja mapendekezo yatatekelezwa. Nchini haiwezi kuendelea ikiwa kuna migawanyiko na utengano wa makabila mengine. Haiwezi kuendelea bila uwakilishi sawa. Sharti tuungane kuziba nyufa kwenye ukuta wa taifa letu,”akaongeza.

Kiongozi wa taifa alisema kila Mkenya anahitaji mwenzake katika safari ndefu ya kushughulikia changamoto zinazolikabili taifa hili kila siku. “Haya ndio mafunzo ambayo mababu zetu walituachia; kwamba tuje pamoja kwa ajili ya kutatua matatizo yetu,” Rais Kenyatta akasema.

You can share this post!

ODM yaomba mbunge wa Maragua msamaha

Maadhimisho Jamhuri Dei 2021: Rais Kenyatta asifia Raila...

T L