• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Washtakiwa kwa wizi wa mitungi ya gesi wakati wa maandamano ya Azimio 

Washtakiwa kwa wizi wa mitungi ya gesi wakati wa maandamano ya Azimio 

Na RICHARD MUNGUTI

HAKIMU Mkuu Francis Kyambia amewaachilia kwa dhamana ya Sh400,000 washukiwa watano wa wizi wa kimabavu.

Bw Kyambia aliwaachilia Alfred Obura, Allan Obonyo, Vincent Onyango, Michael Ooko na Edward Kasee baada ya kukana shtaka la kuiba mitungi 12 ya gesi.

Watano hao walidaiwa kuiba mitungi hiyo siku ya maandamano ya Azimio kulalamikia gharama ya juu ya maisha.

Shtaka hilo, mahakama ilielezwa lilitekelezwa Mei 2, 2023 wakati wa maandamano yaliyoitishwa na kinara wa muungano wa upinzani Bw Raila Odinga.

Walikabiliwa na shtaka la kumnyang’anya Bw Nura Wario mitungi hiyo katika kituo chake cha kuuza mafuta ya petroli cha Shell Petrol kilichoko barabara ya Juja Road, Nairobi.

Mitungi hiyo ya gesi ni ya thamani ya Sh53,500.

Mbali na wizi wa mitungi hiyo ya gesi, washtakiwa wakiwa wamejihami kwa mapanga na fito vya chuma walivunja vioo vya magari yaliyoegeshwa kituoni.

Pia walishtakiwa kwa kuharibu pampu tatu za mafuta zenye thamani ya Sh452,000 za mlalamishi, Bw Wario.

Kesi hiyo itatajwa Juni 2, 2023 kutengewa siku ya kusikilizwa.

  • Tags

You can share this post!

Ezekiel Odero atua jijini Nairobi kuhubiri injili

Swarup Mishra ajiunga na UDA

T L