• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Bunge la Uganda lapitisha mswada tata wa kupambana na ushoga tena bila kuondoa makali yake yaliyopingwa na Amerika

Bunge la Uganda lapitisha mswada tata wa kupambana na ushoga tena bila kuondoa makali yake yaliyopingwa na Amerika

NA AFP

KAMPALA, Uganda

BUNGE la Uganda Jumanne lilipitisha rasimu mpya ya mswada tata wa kupambana na ushoga, huku likidumisha sehemu dhalimu kwenye sheria hiyo kielelezo.

Hii ni licha ya ahadi ya Rais Yoweri Museveni kwamba angefanikisha mabadiliko kwenye mswada huo.

Hii ni kufuatia malalamishi kutoka kwa serikali za mataifa ya Magharibi na makundi ya kutetea haki.

“Mswada ulipita,” Spika wa Bunge Annet Anita Among alisema baada ya awamu ya mwisho ya upigaji kura.

Wabunge wote waliupitisha mswada huo isipokuwa mmoja pekee.

“Tunapaswa kulinda utamaduni wetu. Mataifa ya Magharibi hayawezi kuja kutawala Uganda,” akasema.

Wabunge waliufanyia marekebisho sehemu kadha za mswada huo ili kufafanua kwamba sio hatia kwa mtu kujitambulisha kama shoga.

Lakini kushiriki katika vitendo vya ushoga ni hatia ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani.

Ingawa Museveni alikuwa amewashauri wabunge kuondoa sehemu ya mswada huo inayosema wale wanaopatikana na hatia ya ushoga zaidi ya mara moja watahukumiwa kifo, wabunge walipinga pendekezo hilo.

Hii ina maana kuwa wale ambao watapatikana na kosa la kushiriki ushoga zaidi ya mara moja watapewa adhabu ya kifo.

Adhabu kali kiasi hicho hakijakuwa kikitolewa nchini Uganda kwa miaka mingi.

Mswada huo uliofanyiwa marekebisho unasema kuwa “mtu ambaye ataaminika au kushukiwa kuwa shoga, lakini ambaye hajashiriki ngono na mtu wa jinsi moja, hatatenda kosa la ushoja”.

Rasimu ya awali ya mswada huo pia ulihitaji Waganda kuripoti shughuli za ushoja kwa polisi au afungwe jela kwa miezi sita.

Wabunge walikubali kuifanyia marekebisho sehemu hiyo mnamo Jumanne baada ya Museveni kusema kuwa itashia “kusababisha migongano katika jamii.”

Badala yake, hitaji la kuripoti visa kama hivyo sasa kinahusu madai ya dhuluma za kingono dhidi ya watoto na watu wenye mahitaji maalumu. Adhabu ya kosa hilo sasa imepandishwa hadi kuwa kifungo cha miaka mitano gerezani.

Kulinga na rasimu mpya, mtu yeyote ambaye “kwa atuvumisha ushoga kimakusudi” atapewa adhabu ya miaka 20 gerezani.

Sehemu hiyo haijabadilisha kutoka kwa rasimu ya mswada wa awali.

Mashirika ambaye yatapatikana na hatia ya kuhimiza shughuli za ngono za jinsia moja yatapigwa marufuku kwa kipindi cha miaka 10.

Frank Mugisha, Mkurugenzi wa Shirika la Sexual Minorities Uganda, linatetea haki za mashoga na ambayo shughuli zake zilisimamisha mwaka jana, alisema kupitishwa kwa mswada huo kunahatarisha maisha ya mashoga na wasagaji nchini humo.

“Kuna mkanganyiko kwa sababu sheria hiyo kielelezo inasema kuwa unaweza kuwa shoga lakini hauwezi kusema lolote kuihusu,” akaambia shirika la habari la AFP.

Aliongeza kuwa kupitishwa kwa mswada huo na idadi kubwa ya wabunge kunaonyesha kuwa “wabunge wanalenga kuweka maisha ya mashoga hatarini kimakusudi.”

Mswada huo sasa utawasilishwa kwa Rais Museveni, ambayo kwa mara nyingine anaweza kutumia mamlaka yake kwa kukosa kuutia saini au hautie saini kuwa sheria kamili.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Isaac Ruto ateuliwa mwanachama wa JSC kuwakilisha umma

Uchumi: Mahasla walemewa

T L