• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Faraja ulimwenguni baada ya Amerika kufungua mipaka yake kwa wageni

Faraja ulimwenguni baada ya Amerika kufungua mipaka yake kwa wageni

Na AFP

WASHINTON, Amerika

AMERIKA Jumatatu ilifungua mipaka yake kwa wageni ambao wamepata dozi zote za chanjo ya kuzuia Covid-19. Kuondolewa kwa marufuku hiyo, iliyowekwa miezi 20, inatoa nafasi kwa familia na marafiki kuungana pamoja baada ya kutengana kwa zaidi ya miezi 20.

Mafuruku hiyo iliwekwa na Rais wa zamani Donald Trump mapema 2020 na ikadumishwa na Rais wa sasa Joe Biden. Baada ya tangazo hilo kutolewa, wasafiri katika viwanja katika mataifa mbalimbali ya bara Ulaya walipiga foleni kukanunua tiketi za kuwawezesha kusafiri Amerika.

Vile vile, foleni ndefu ya wananchi waliovalia barakoa na magari yalionekana alafajiri katika mipaka ya Amerika na Mexico na Canada. Amerika ilifunga mipaka yake kuanzia Machi 15, 2020 kwa wasafiri kutoka maeneo mbalimbali ya dunia yakiwemo mataifa ya wanachama wa Umoja wa Ulaya, Uingereza, China, India na Brazil.

Hii ni katika juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona vilivyoangamiza watu wengi zaidi nchini humo.Wageni kutoka mataifa jirani ya Mexica na Canada walizimwa kuingia Amerika.

You can share this post!

AC Milan na Inter Milan nguvu sawa katika gozi la Serie A

Kimemia apuuzilia mbali madai kuwa magavana wanashurutishwa...

T L