• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:01 AM
AFYA: Fahamu jinsi unavyoweza kuzuia lehemu mbaya

AFYA: Fahamu jinsi unavyoweza kuzuia lehemu mbaya

NA MARGARET MAINA

[email protected]

ILI kupunguza viwango vyako vya lehemu mbaya, fuata mtindo wa ulaji unaozingatia afya bora.

Hii ina maana ya kuchagua aina ya vyakula safi na ambavyo havijachakatwa, na kupunguza mafuta yasiyo na tija kwa afya, chumvi mbaya na sukari iliyoongezwa.

Mtindo wa ulaji unaozingatia afya ya moyo una wingi wa nafaka, nyuzinyuzi, vitamini, madini na mafuta yenye afya.

Baadhi ya sababu za lehemu ya juu ni pamoja na:

–         Ulaji mwingi wa vyakula vilivyo na mafuta yasiyofaa kama vile nyama ya mafuta, siagi, krimu, na vyakula vingi vya kukaanga na bidhaa za kuoka za kibiashara (kama vile kama mikate, biskuti, na keki).

–         Ulaji mdogo wa vyakula vyenye mafuta yenye afya – mafuta yenye afya huongeza lehemu nzuri. Vyakula vyenye mafuta yenye afya ni pamoja na parachichi, karanga, mbegu, zeituni, mafuta ya kupikia yaliyotengenezwa kwa mimea au mbegu, na samaki.

–         Ulaji mdogo wa vyakula vyenye nyuzinyuzi – vyakula ambavyo vina nyuzinyuzi nyingi za lishe, haswa nyuzi mumunyifu, vinaweza kupunguza kiwango cha lehemu mbaya.

  • Viwango vya chini vya shughuli za mwili na mazoezi.
  • Kuwa na uzito mkubwa au unene kupita kiasi na kuwa na mafuta mengi mwilini.
  • Kuvuta sigara kunaweza kusababisha viwango vya juu vya lehemu.
  • Jenetiki – historia ya familia yako inaweza kuathiri kiwango chako cha leemu.

Katika baadhi ya familia, watu kadhaa wanaweza kugunduliwa na lehemu ya juu au ugonjwa wa moyo katika umri mdogo.

Tunachokula huathiri viwango vyetu vya lehemu na inaweza kusaidia kupunguza hatari yetu ya magonjwa.

Mtindo wa kula kwa afya ni pamoja na:

–         Mboga nyingi, matunda na nafaka nzima

–         Aina mbalimbali za vyakula vyenye afya vyenye protini nyingi (hasa samaki na dagaa), kunde (kama vile maharagwe na dengu), karanga na mbegu. Kiasi kidogo cha mayai na nyama nyeupe pia kinaweza kujumuishwa katika muundo wa ulaji wa afya ya moyo.

–         Maziwa yasiyo na ladha, mtindi na jibini. Watu wenye lehemu ya juu wanapaswa kuchagua aina za mafuta zilizopunguzwa.

–         Mafuta yenye afya. Chagua karanga, mbegu, parachichi, mizeituni na mafuta yake kwa kupikia

–         Mimea na viungo kwa vyakula vya ladha, badala ya kutumia chumvi.

–         Punguza au epuka nyama iliyochakatwa ikiwa ni pamoja na soseji na nyama ya deli (kama vile ham, bekoni na salami)

  • Tags

You can share this post!

Faida za kiafya zipatikanazo ukinywa chai ya mnanaa

Kaunti yaombwa ichapishe nakala kwa Kiswahili

T L