• Nairobi
 • Last Updated December 4th, 2023 7:22 PM
AFYA NI MTAJI: Dalili hizi huenda zikaashiria una kansa ya matiti

AFYA NI MTAJI: Dalili hizi huenda zikaashiria una kansa ya matiti

NA WANGU KANURI

KANSA ya matiti hutokea baada ya kuota kwa uvimbe unaosababisha kuchipuka kwa seli katika sehemu ya ndani ya matiti.

Mmoja kati ya wanawake wanane wako katika hatari ya kuathirika na ugonjwa huu maishan.

Ni nini kinachosababisha kansa ya matiti?

Licha ya kuwa hakuna utafiti kamili unaoonyesha ni nini hasa kinachosababisha maradhi haya, kunazo sababu zinazoongeza uwezekano wa kuathirika. Baadhi yake sababu hizo ni;

 • Umri: Unapozidi kukomaa ndivyo hatari ya kukumbwa na maradhi haya inavyozidi kuongezeka. Inaaminika kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya visa vya kansa ya matiti, huripotiwa na wanawake zaidi wenye umri wa miaka 50.
 • Historia ya familia: Ikiwa mojawapo wa jamaa zako katika familia amewahi kuathirika na maradhi haya, basi hali hii inaongeza uwezekano wako wa kuathirirka
 • Unywaji wa pombe: Wanawake wanaokunywa pombe kwa wingi huwa katika hatari ya kuathirika na ugonjwa huu, wakilinganishwa na wasio tumia vinywaji hivi.
 • Uamuzi wa upangaji uzazi: Wanawake wanaoamua kutopata watoto au wanaozaa baada ya kutimu umri wa miaka 30, huwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu.
 • kiwa umewahi pokea matibabu kukabiliana na ugonjwa huu, basi pia wewe uko katika hatari ya kuathirika.

Ili kupunguza uwezekano wa kukumbwa na ugonjwa huu, unapaswa kuchukua hatua zifuatazo:

Kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kwenye matiti kila mara.

Wanawake wanapaswa kujua historia kuhusu ugonjwa huu katika familia yao

Ishara za saratani ya matiti

 • Uvimbe usio na uchungu katika shemu ya ndani ya matiti
 • Joto katika sehemu ya matiti
  Hali isiyo ya kawaida kwenye chuchu
 • Uchungu kwenye chuchu.
 • Sehemu ya matiti kubadili rangi na kuwa nyekundu
 • Titi kuwa kubwa
 • Kutokwa na majimaji yaliyochanganyika na damu
 • Uchungu kwenye matiti usiohusishwa na kukaribia kwa siku za hedhi
 • Kutokwa na uvimbe kwenye makwapa

Licha ya kuwa ishara hizi huhusishwa na saratani ya matiti, kuna uwezekano wa kutoshuhudia dalili hizi ilhali umeathirika.

 

 • Tags

You can share this post!

Polisi lawamani tena kwa kifo cha raia

Man-U wanaweza kumaliza nne-bora EPL?

T L