• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
AKILIMALI: Alikuwa jamaa la kubeba mizigo; sasa ana biashara yake ya matikitimaji

AKILIMALI: Alikuwa jamaa la kubeba mizigo; sasa ana biashara yake ya matikitimaji

Na PATRICK KILAVUKA

BAADA ya Shule ya Upili, Samuel Ndungu alianza kubebea watu na wachuuzi mizigo nia ikiwa kupata hela ambazo zingemkimu kimaisha.

Alisomea Shule ya Msingi na Sekondari ya Murang’a High.

Kwa miezi sita, anasema aliweka pesa ambazo alizitumia kama mtaji wa kuanzisha biashara ya kuuza matikitimaji katika soko la Marikiti, jijini Nairobi.

Alianza na mtaji wa Sh30,000.

Akawa anauza kilo 100 na sasa anaagiza tani 10-15 kutoka Tanzania, Uganda na humu nchini hususan Mwingi, Kajiado na Mombasa.

Amefanya biashara hii kwa miaka kumi.

Wakati huo, alikuwa anauza kilo kwa Sh25 lakini sasa anaiuza Sh35.

Sababu iliyomfanya kuuza matikitimaji ni kwamba, aliona ni matunda yanayopendwa sana na yanaweza kumpatia riziki ya kila siku mbali na kuwa na kiu ya kufanya biashara hii akiwa shuleni.

Japo inaleta mapato kwa haraka, anasema ina changamoto ya kuharibika kwa haraka na inatakiwa kubebewa kwa uangalifu na gharama za usafiriaji na uagizaji ni za juu.

Pia, kuna wateja ambao wanataka kuuziwa kwa bei ya chini ingawa huwazungumzia kwa upole kuelewa kwa nini anauza kwa bei hiyo.

Wakati yanapoadimika, gharama huwa za juu zaidi hali ambayo hubidi bei kupanda.

Wateja wake wanatoka Nairobi na ukanda wa jiji.

Je, yeye hutambuaje tikitimaji nzuri?

“Ukiliangalia huwa angavu sana na likikatwa kipande, utapata ni tamu ukionja,” anasema.

Kutokana na kazi yake, ameajiri wafanyakazi wawili ambao wanamsaidia kuuza.

Kazi hii ambayo ilimwezesha kujiajiri, anasema imekuwa kitega uchumi kwake na inamfaidi kwa kuweka mkate mezani kila jioni, kujikimu, kujistawisha na kwa matakwa mengineyo ya maisha.

Ushauri wake ni kwamba, kama angedharau mwanzo mdogo wa kazi yake, labda hangefika umbali huu.

Hivyo basi, anawashauri vijana wanaomaliza shule na vyuo kuwa wabunifu kimaisha ili, watie kitu mfukoni kuliko kungojea tu waajiriwe ilhali wanaweza kujiajiri kwa kutumiwa maarifa waliyopata masomoni kujiendeleza kimaisha.

La muhimu ni bidii na watapata mapato ya kufuaulu maishani.

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Ndizi za kienyeji zinazopendwa kwa sukari yake

WASONGA: Likizo si suluhu, ni sawa na kutibu malaria na...

T L