• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 12:33 PM
Rose Muhando akanusha kutapeli kanisa la mwimbaji Mkenya Ali Mukhwana Sh200,000

Rose Muhando akanusha kutapeli kanisa la mwimbaji Mkenya Ali Mukhwana Sh200,000

NA SINDA MATIKO

MWANAMUZIKI wa injili Rose Muhando kakanusha kutapeli kanisa la mwimbaji wa injili Ali Mukhwana Sh2o0,000.

Siku chache zilizopita, Mukhwana alidai kanisa lao lilimlipa Muhando fedha hizo kwa ajili ya shoo kwenye mkutano wao wa Bungoma lakini mwimbaji huyo akaingia mitini.

Kwenye video iliyotundikwa mitandaoni, mwimbaji huyo huyo anasema alishangazwa na hatua ya Muhando kujiandikisha kwa shoo mbili kwa wakati mmoja huku akimlaumu kwa ‘kula nauli’.

“Nilishangaa kuona mabango ya Muhando ya mkutano mwingine, ilhali alikuwa ashakubali kuja mkutano wetu wa Bungoma mpaka hata tukamtumia pesa. Ilibidi nipigie pasta aliyekuwa anahusika na mkutano huo mwingine kumuuliza kwa nini ana picha za Muhando ambaye anapaswa kuja kwa shoo yetu. Pasta huyo akaniambia kwamba hata wao walishamtumia laki mbili,” akasema Mukhwana.

Aliongeza kudai kwamba baadaye zikiwa zimebaki siku tatu hivi kabla ya shoo, akampigia tena Muhando na hapo ndipo alimwambia kwamba alikuwa mgonjwa.

“Aliniambia, Ali, saa hizi niko mgonjwa. Nikamuuliza, mgonjwa wapi? Akanijibu, nina jipu mahali ambapo siwezi kuelezea,” Mukhwana alisema huku waumini waliokuwa wakimzingira wakitikisa vichwa.

Alihitimisha shutuma hizo akimtaja kuwa ‘mtu mwongo aliyekula fare (nauli)’.

Sasa baada ya kutua Kenya, Desemba 6, 2023 Muhando ameamua kunyoosha mambo.

“Kuhusu stori hizo mlizoziskia siku mbili tatu zilizoongelewa na Ali Mukhwana sio kweli. Aliyenialika ni Nathaniel Maina na ndio alikuwa mwenyeji wa mikutano yote mitano niliyohudhuria na Mukwana akinipigia simu nilikuwa mikononi mwa mchungaji huyu Nathaniel Maina,” Muhando anasema.

Staa huyo anakiri kwamba ni kweli Ali alimwalika kwenye mkutano wao Bungoma.

“Ni kweli Ali alinialika lakini ni kulingana na sababu mbaya sana ambazo siwezi kuzielezea sikuweza kufika (Bungoma). Sitaki kusema tulibishania nini maana sikuja hapa kwa mashtaka. Alinialika na niliposhindwa kwenda mkutano nilirudisha pesa yao ambayo yeye anasema ni 200,000 sio kweli ilikuwa ni Sh50,000 na nina ushahidi huo.”

Kulingana na Rose, maagano ya malipo yalikuwa Sh170,000 huku Sh50,000 walizotuma na akazirejesha baada ya kushindwa kufika.

Aidha alikana kuwatapeli wachungaji wengine watano kama alivyodai Ali huku akisema kuwa kamsamehe.

  • Tags

You can share this post!

Hivi unazijua skendo za ‘Papa Mokonzi’ Koffi...

Machogu: Usahihishaji KCPE ulikuwa kazi safi na wakuu wa...

T L