• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
DOMO: Huku kuanika tumbo kwasinya

DOMO: Huku kuanika tumbo kwasinya

NA MWANAMIPASHO

KUNA wimbo wa zilizopendwa niliosikiliza juzi, ukanikuna akili.

Sijui jina la wimbo ila najua wasanii walotunga wanaitwa Jamnazi Afrika.

Ubeti ulionikosha kwenye wimbo huo unaenda hivi.

“Mimi ninalo jambo lanisumbua akili, ulimwengu umepasuka mahali. Mungu alipanga usiku saa ya kulala, mbona walimwengu mumebadili mipango. Usiku sasa umegeuka mchana na mchana ni kama usiku jamani eeeh! Mi nashangaa!”

Hapo kwenye kushangaa, kuna jambo linanisumbua akili. Hivi huu utamaduni wa mademu kila wakipachikwa mimba, wanaposti kutuonyesha matumbo yao, umetoka wapi?

Ni kwa nini wanawake wamesahau suala zima la kujisitiri. Sasa hivi kila celeb akipachikwa ujauzito lazima aturingishe tumbo lake utadhani tuna haja ya kujua. Wengine wanaonichosha ni wale wanaoposti wakiwa tumbo wazi. Huwa malengo ni nini haswa? Kwamba ni ushahidi wa kuwa mlishiriki ngono? Au mnaspoti tuone mlivyo na mbegu za kutosha? Au mnaposti tuwasifie? Kusema kweli sielewi.

Juzi kaposti kitumbo chake rafiki yangu Careh Priscillah baada ya kunasa ujauzito wa pili. Kusema kweli sikufurahia kabisa. Sio kwa kitumbo kama hicho halafu unaamua kuposti ukiwa umevalia bikini jamani? Mambo haya mumeiga kutoka wapi? Mnaona sifa kweli? Mnaona tutafurahia? Sisi hayatuhusu. Wewe kupachikwa mimba na dume lako inatuhusu nini? Dada, kipindi akikukanyaga kitandani mbona haukuposti basi tuone jembe lake linavyojua kulima.

Wengine mnaposti wakati miili yenu inaonekana kukosa afya. Wapo nilioona na badala ya kupata picha ya binti mjamzito, picha niliyopata ni ya mtoto anayeugua Kwashiakor. Halafu mkichambwa mnaanza kusema, watu wanawaonea wivu na chuki? Wivu gani sasa. Chuki gani. Hivi mnadhani nyie ndio wanawake wa kwanza kunasa ujauzito?

Mtoto wa kwanza au wa pili, mwatuhangaisha na mapicha kibao mitandaoni kama vile tunajali. Mimba zenu zinatuhusu nini, nauliza. Sasa mngelikuwa kama mama zetu wengine waliojaliwa kushika ujauzito mara 10, itakuwaje.

Kwangu mimi, picha au video zile hasa za mwanamke akiwa nusu uchi wakati ni mjamzito huwa ni kero.

Pana haja na maana ya kujisitiri. Ndio sababu hutaona tabia hizi za kishamba na mademu wa Kiislaamu. Sababu wanaheshimu miili yao. Wanatambua thamani yao kama wanawake. Miili yao sio ya kuonwa na kila mtu. Nyie kina Careh mnaona sifa sana.

Sasa kesho ujauzito ukiharibika, nina uhakika, mtakuja kukenua meno mkidai eti ni kwa sababu mlisemwa vibaya.

Kuna thamani kubwa kwa kuwa msiri kwa mambo kama haya. Umeolewa, unaona sifa gani kuja kutuonyesha litumbo lote hilo. Tulia, jifungue mlee mwanao kimya kimya. Mnasinya. Sheeeh!

You can share this post!

Montreal ya Wanyama kuwania tiketi Jumapili nayo...

Onyo ukame utaongeza kipindupindu

T L