• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:55 AM
JIFUNZE BIASHARA: Ya kuzingatia wakati wa kutengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa

JIFUNZE BIASHARA: Ya kuzingatia wakati wa kutengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa

NA PETER CHANGTOEK

WAKATI wa kutengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa, kama vile gururu, kuna mambo yanayofaa kuzingatiwa.

Usafi ni jambo la kwanza, ili kuzuia kuharibika kwa bidhaa, na hata kuwadhuru wateja.

Kwa mujibu wa Kevine Otieno, mtaalamu wa kilimo kutoka katika Chuo Kikuu cha Egerton, ni kwamba, gururu huharibika hususan endapo gesi itakuwako kwa bidhaa hiyo.

Aidha, anasema iwapo gururu itakuwa nyepesi na kuachana, itaharibika.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, gesi hiyo husababishwa na kutozingatiwa kwa usafi unaotakikana, ilhali kuachana na kuwa nyepesi kwayo, husababishwa na kutozingatia mchakato unaofaa kuzingatiwa wakati wa utengenezaji.

“Pia, kama gururu haijakuwa nzito wakati wa mchakato wa kutengeneza, basi ubora wa maziwa yanayotumiwa unafaa kuzingatiwa. Hii inaweza kusababishwa na viuabakteria ambavyo vinaweza kuwa kwa maziwa, ambavyo vinaweza kuua bakteria zinazotakikana ili mchakato wa kuchacha kwa maziwa ufanyike,” aeleza.

Aidha, mtaalamu huyo anasema kuwa, kuongeza sukari nyingi wakati wa kutengeneza bidhaa za maziwa kutaharibu bidhaa zenyewe.

“Zingatia usafi kwanza. Hakikisha kwamba maziwa yanakamuliwa kutoka kwa ng’ombe wasiokuwa na magonjwa. Viuabakteria nilivyoelezea vinapatikana kwa ng’ombe anayeendelea kupata matibabu. Pia, hakikisha kuwa ng’ombe wanakula lishe safi, kunywa maji safi na kulala mahali safi. Maziwa yafaa kuhifadhiwa katika mahali safi na mhudumu awe nadhifu,” aongeza.

Anasema kuwa, mchakato wa kutengeneza bidhaa za maziwa haufai kuharakishwa, bali bidhaa zinafaa kutengenezwa kitaratibu.Mtaalamu huyo anaongeza kuwa, anayenuia kuanza kuzitengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa, ni lazima awe na leseni zinazohitajika kutoka kwa mamlaka simamizi.

  • Tags

You can share this post!

Mara mbili akila hasara lakini bado anang’ang’ana

ZARAA: Juhudi za kutema ukuzaji tumbaku zaanza kufaulu

T L