• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Mwanasaikolojia Faith Gichanga ataka kampuni, watu binafsi kuchukulia kwa uzito huduma za ushauri nasaha

Mwanasaikolojia Faith Gichanga ataka kampuni, watu binafsi kuchukulia kwa uzito huduma za ushauri nasaha

NA MAGDALENE WANJA

MARUFUKU ya usafiri na kwenda kazini yaliadhiri watu wengi kisaikolojia wakati wa kanga la Covid-19.

Baadhi ya wafanyakazi walijipata katika hali ngumu zaidi haswa baada ya kuwapoteza wapendwa wao na mali.

Kulingana mwanasaikolojia Bi Faith Gichanga, mabadiliko hayo ambayo yalirekodi hali tofauti ya mazingira yalichangia pia katika msongo wa mawazo wa watu wengi.

Mwanasaikolojia Faith Gichanga ataka kampuni, watu binafsi kuchukulia kwa uzito huduma za ushauri nasaha. PICHA | MAGDALENE WANJA

Waajiri ambao walijitolea katika kuwatafutia wafanyakazi wao huduma za ushauru wa kisaikolojia waliweza kuokoa muda wa kuweza kurejesha hali zao za hapo awali.

“Idadi ya watu waliotaka huduma hizi iliongezeka sana wakati wa janga hilo na hata baada yake,” anasema Bi Gichanga.

Bi Gichanga anaongeza kuwa ni muhimu kwa mashirika na kampuni kuwarahisishia wafanyakazi wao mzigo wa kutafuta huduma hizi.

Mwanasaikolojia Faith Gichanga. Lengo lake kuu ni kuhakikisha kuwa mazingira ya kazini yanazingatia afya ya wafanyakazi. PICHA | MAGDALENE WANJA

Huduma hizi hutozwa kati ya Sh3,000 na Sh20,000. Ada hizi hutegemea kama ni watu binafsi au makundi ya watu wengi.

Bi Gichanga anaongoza kuwa ingawa huduma za ushauri wa kisaikolojia ni muhimu kwa afya ya binafamu haswa kazini, bado hazijachukuliwa kwa uzito unaostahili.

  • Tags

You can share this post!

Mtaalam anayewashauri wagonjwa jinsi ya kutumia vifaa vya...

Muuzaji ngozi taabani kwa kuhepa polisi miaka 3

T L