• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Bado nasubiri jibu la demu miaka 2 sasa!

Bado nasubiri jibu la demu miaka 2 sasa!

Salamu shangazi. Nina huzuni nyingi moyoni kuhusu mwanamke ninayempenda. Nilimwambia wazi kuwa nampenda na amenihangaisha kwa miaka miwili akiniambia atanijibu.

Mtu hahitaji miaka kujua iwapo ana hisia kwa mwingine au la. Inawezekana kwamba mwanamke huyo hakupendi lakini anahisi vigumu kukwambia. Sasa ni juu yako kuamua kama utaendelea kungoja ama utaachana naye.

Akiwa mbali namtamani akija karibu simpi mahaba!

Uhusiano wangu wa kimapenzi umeingia baridi kutokana na hali yangu. Nikiwa mbali naye huwa na hisia nzito za kimapenzi kwake lakini akihitaji huduma za chumbani ninashindwa.

Huenda hali hiyo inatokana na kwamba huna mazoea ya kushiriki mahaba na pia huamini una uwezo wa kumtosheleza mpenzi wako. Unahitaji kumtembelea mtaalamu wa afya ya uzazi uone kama atakusaidia.

Ananilaumu eti nimepata mimba mapema, sielewi

Nimeolewa miezi mitatu iliyopita na tayari nina mimba. Sasa mume wangu anataka kuniacha akidai hakutaka mtoto haraka . Nahisi anilaumu bure.

Makosa si yako bali ni ya mume wako. Angekuelezea mpango wake ili mshauriane kuhusu jinsi ya kuzuia mimba. Jaribu kushauriana naye. Siamini anaweza kukuacha kwa sababu hiyo.

Sijui iwapo kweli nampenda

Kuna mwanamke tunayefanya kazi naye na tumekuwa marafiki kwa miezi kadhaa sasa. Nahisi kama nampenda lakini sina hakika. Nishauri tafadhali.

Ninaamini hisia zako za kimapenzi kwa mwanamke huyo zimetokana na urafiki wenu. Usiweke wazi hisia zako kwake kama huna hakika. Badala yake, dumisha urafiki huo hadi utakapothibitisha kuwa unampenda kwa dhati.

  • Tags

You can share this post!

Mackenzie hubomoa chakula sawasawa akiwa kizuizini,...

Gor yarejea kileleni baada ya Tusker kulewa magoli ya Wazito

T L