• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Jinsi ya kudumisha usafi wa ndani ya chumba chako cha kulala

Jinsi ya kudumisha usafi wa ndani ya chumba chako cha kulala

NA MARGARET MAINA

[email protected]

UNAHITAJI chumba cha kulala ambacho ni nadhifu ili uwe na utulivu unapopumzika ama peke yako au na yule umpendaye.

Hiki ni chumba ambacho kimetengwa kwa ajili ya kukusaidia kuondoa uchovu mara baada ya siku ndefu yenye shughuli za hapa na pale.

Ingawa kinaweza kuwa chumba cha faragha, usikigeuze mahali pa kutupia taka au pa kuzulia fujo za kila aina.

Ukikigeuza chumba hiki kuwa ni jaa la taka, basi unapoenda kulala itakuwa ni sawa na wewe kujaribu kuenda kulala msituni.

Chukua dakika moja na uchore taswira ya jinsi ulivyotaka chumba chako kionekane na jinsi ulivyofikiria ungekuwa ukihisi ukiingia chumbani humo kila usiku au wakati wowote ukitaka kujituliza.

Ni muhimu kwako wewe kuhakikisha chumba cha kulala ni nadhifu kwa sababu kadhaa.

Wewe ni mtu wa maana

Chumba chako cha kulala kikiwa nadhifu na chenye mpangilio wa kipekee kitasaidia kuboresha afya yako ya kiakili na kihisia. Kinaweza hata kusaidia kuimarisha ndoa yako unapokitambua kuwa ni sehemu ya kukuepusha kidogo na mafadhaiko na machafuko yanayoendelea katika ulimwengu wako wote.

Unaweka mipaka 

Hiki si chumba ambacho anaingia kila mtu. Aghalabu unaweza kudhibiti chumba chako cha kulala ukilinganisha na chumba kingine chochote ndani ya nyumba yako. Chumba chako cha kulala ni chako (pamoja na mchumba wako). Kwa hivyo unaweza kupiga marufuku vinyago na “vitu” vingine ambavyo havipaswi kuhifadhiwa humo. Fanya hivyo ili iwe rahisi wewe kukisafisha.

Kinakupa faraja wakati unahitaji utulivu

Chumba cha kulala kilicho na vitu vingi kinakatisha tamaa na kuchangia sana hisia za wasiwasi na unyogovu.

Unapaswa kuwa na angalau sehemu moja katika nyumba yako ambapo ukiwa pale unakuwa na amani.

Unahitaji nafasi ambayo unaweza kuenda kwa ajili ya kujituliza kihisia.

  • Tags

You can share this post!

Mwanasiasa Githurai ajitia kitanzi

Ajabu maiti ikifufuka Ecuador

T L