• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:20 AM
Mume wangu na meidi wanatumiana SMS za siri

Mume wangu na meidi wanatumiana SMS za siri

SHANGAZI AKUJIBU:

Ninashuku mfanyakazi wangu wa nyumbani ana uhusiano na mume wangu. Nimekagua simu yake na kugundua wamekuwa wakiwasiliana. Naona aibu kumuuliza mume wangu. Nifanyeje?

Ni wazi kuwa wawili hao huwa hawazungumzi kuhusu kazi. Kuna uhusiano mwingine kati yao. Jinsi pekee ya kuutibua ni kumfuta kazi mara moja. Hatua hiyo pia itamuingiza baridi mume wako kwani atajua umegundua.

Mke wa mchungaji ananitaka kimapenzi

Nina miaka 26 na ninahudumu katika kanisa langu. Nilishangaa juzi mke wa pasta wetu aliponiita faraghani akaniambia ananipenda na anataka tuwe na mpango wa kando. Nifanye nini?

Mke wa pasta ana hisia sawa na wengine. Lakini mpango wake huo ni kinyume na maadili ya ndoa, usaliti dhidi ya mume wake na hatari kwa maisha yako. Usikubali.

Mke anapika tu mashendea!

Huu ni mwezi wa tatu katika ndoa. Nampenda mke wangu lakini ana upungufu fulani. Hajui kupika. Mamangu ni mpishi hodari na nilikuwa nimezoea chakula chake. Nifanyeje?

Ujuzi wa mambo hutokana na mafunzo. Shauriana na mke wako kwa upole kuhusu jambo hilo. Kama una uwezo wa kifedha, mpeleke katika chuo cha mafunzo ya upishi.

Nimekutana na picha za ngono kwa simu ya binti

Nimegundua binti yangu mwanafunzi wa shule ya upili anatumia wakati wake mwingi kutazama filamu za ngono katika simu yake. Nimeshtuka sana, naomba ushauri wako.

Ni lazima uchukue hatua haraka kabla binti yako hajazama zaidi katika uraibu huo. Wewe ndiye umenunulia simu hiyo. Mwambie wazi hutakubali aitumie kwa mambo kama hayo la sivyo uichukue.

  • Tags

You can share this post!

Hatutabebwa na ‘tam tam’ za Ruto, magavana wahakikishia...

Owalo awataka wabunge kubadilisha sheria na sera za sekta...

T L