• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
Tabia na mambo ya kuepuka asubuhi

Tabia na mambo ya kuepuka asubuhi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

JE, unajua kwamba jambo la kwanza unalofanya asubuhi linaweza likakuamlia jinsi siku yako nzima itakavyokuwa?

Utaratibu wa asubuhi unaweza kukutengenezea au kukuharibia mpangilio wa matumizi ya muda wako katika siku husika.

Mambo ya kwanza unayofanya asubuhi ni muhimu yawe yanayoweza kuibua mtazamo chanya wa maisha, kuleta tija, utulivu au msisimko mwingine wowote unaohitajika.

Msichana akikimbia asubuhi jua likichomoza. PICHA | MAKTABA 

Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu hushiriki katika vitendo au tabia zisizofaa ambazo huharibu bila kukusudia sehemu zinazofuata za siku mahsusi.

Jifunze ni nini cha kufanya kwanza asubuhi ili kuanzisha utaratibu thabiti na kuunda ufahamu wenye manufaa ambao unatosha siku nzima.

Tabia za kuepuka asubuhi

Iwapo unatazamia kuongeza tija na kujisikia vizuri mara tu siku inapoanza, hakikisha unaepuke tabia hizi asubuhi.

  • Kubonyeza kitufe cha kuahirisha saa zaidi ya mara moja

Kuahirisha mara moja kunaweza kugeuka kwa urahisi kuwa mara tano na pia kwa kufanya hivyo utakuwa unafundisha ubongo kuahirisha kuamka.

Ingawa unaposikia sauti ya kengele ya saa wakati mwingine unahisi kama umepigwa na tofali asubuhi, kuibuka kutoka kitandani wakati unaofaa bila kubonyeza kitufe hukuchangamsha siku nzima.

  • Kuangalia simu yako bila mpango

Kuangalia simu yako, kujivinjari kwenye mitandao ya kijamii, na kuangalia baruapepe unapoamka ni jambo moja baya zaidi kufanya isipokuwa tu ikibidi au wakati wa dharura. Si tu kwamba ukifanya hivyo utakuwa unajaza ubongo na habari nyingi kupita kiasi, lakini pia unaweza kuweka akili kwa ulinganisho na ulinganuo wa mawazo ya huzuni au ya wasiwasi.

  • Kuwasha runinga

Kutazama runinga punde tu unapoamka kunaleta madhara sawa na yamayoletwa na kuvinjari mitandao ya kijamii asubuhi. Unaweka mtazamo na mawazo yako katika hatari zaidi. Unachoona, kusikia na kuhisi asubuhi kinaweza kukaa ndani ya ufahamu wako siku nzima.

Hatimaye, ikiwa maudhui ni hasi, hii inaweza kuwa tatizo na kuweka toni hasi kwa siku.

  • Kutumia sukari iliyosafishwa

Ulaji wa sukari iliyosafishwa mara moja husababisha kupanda kiwango cha sukari kwenye damu kwa siku nzima. Sukari iliyosafishwa mara nyingi huwa katika vyakula vya kiamsha kinywa unavyopenda kama vile nafaka, donati, keki na kadhalika.

Kile unachokila kama kiamsha kinywa kinaweza kuathiri hisia na chaguzi zinazofuata kwa siku nzima. Hii ndiyo sababu wataalamu wengi wa afya wanapendekeza kifungua kinywa kiwe ni mlo muhimu zaidi wa siku.

  • Kunywa kahawa kabla ya maji

Mwili tayari umepungukiwa na maji baada ya kuamka na kunywa kahawa yenye kafeini mara moja ni hatua isiyofaa.

  • Kukimbilia kujitayarisha

Kuanza siku katika hali ya hofu kunaweza kuathiri mfumo wa neva na kutolewa kwa homoni ya mafadhaiko. Utabaki katika hali ya tahadhari kwa saa nyingi baada ya hali ya mkazo. Msongo wa mawazo huathiri afya ya kiakili, kihisia na kimwili kwa njia zenye athari hasi au chanya.

  • Kuketi kwa muda mrefu sana

Kwa sababu mwili hupungukiwa na maji mwilini baada ya kulala, viungo na misuli huhisi kukakamaa na kukaa kwa utulivu kwa muda mrefu sana huongeza hali hii. Ingawa ni mbaya zaidi asubuhi, kukaa kwa muda mrefu sana hakufai kuelekeza afya ya kimwili au ya kiakili pia.

  • Tags

You can share this post!

Ole wenu mliomtamani, Akothee aoleka na mchumba wake mzungu

Gwiji wa sataranji

T L