• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:29 PM
UJAUZITO NA UZAZI: Kuongeza madini ya chuma mwilini

UJAUZITO NA UZAZI: Kuongeza madini ya chuma mwilini

Na PAULINE ONGAJI

UPUNGUFU wa madini ya chuma una madhara kwa wanawake wajawazito.

Kwa mfano tatizo hili husababisha maradhi ya anemia. Licha ya kuwa ugonjwa huu huwa umekithiri wakati wa ujauzito, ni nadra sana kwa wajawazito kupatikana na hali hii katika kipindi cha wiki 30 za ujauzito.

Anemia huathiri wengi baadaye katika ujauzito ambapo kijusi huhitaji zaidi virutubisho vya madini ya chuma. Madini ya chuma ni muhimu sana katika kuota kwa mfumo wa neva. Kwa mfano, ni muhimu kwa seli za nyuroni (neurons) zinazounda mwunganisho na nyingine kuweka safu ya ulinzi nje ya seli za neva zinazoimarisha usambazaji wa ishara.

Viwango vya chini vya madini ya chuma kunawaweza kusababisha matatizo ya kukua. Utafiti umeonyesha kwamba watoto wanaozaliwa na akina mama walio na anemia, huwa wadogo na wana uwezekano wa kuzaliwa kabla ya muda kamili.

Wakati wa ujauzito unahitaji miligramu 27 za virutubisho vya chuma kila siku. Kwa hivyo kuna vyakula ambavyo unapaswa kula ili kuongeza viwango vya madini hii mwilini, kama vile nyama, kuku na mayai. Aidha, unapaswa kula vyakula vya jamii ya maharagwe kwa wingi.

Mbali na hayo, kuna vijalizo vya virutubisho vya chuma ambavyo mjamzito anaweza tumia ili kuimarisha viwango vya madini haya mwilini. Lakini kabla ya kutumia bidhaa yoyote ile, sharti uwe umependekezewa na daktari.

You can share this post!

Mvua kunyesha nchini Januari 15 hadi 19, yasema idara ya...

Lempurkel ashtakiwa upya kwa matamshi ya uchochezi

T L