• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 7:50 AM
JUMA NAMLOLA: Kuna maisha baada ya sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya, tutahadhari

JUMA NAMLOLA: Kuna maisha baada ya sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya, tutahadhari

Na JUMA NAMLOLA

Kila anayesoma makala haya hana budi kurudisha shukrani kwa Muumba wake kumfikisha siku ya mwisho ya mwaka 2021.

Si kwa ujanja wa wanadamu kwamba Wakenya tumevuka viunzi vingi.

Tumepambana na Corona tangu ikiwa haina jina, ikaitwa Covid-19, ikawa na vijina kama Delta, na sasa kwa mapenzi ya Mungu, hata wimbi la Omicron linatuacha tuuone mwaka wa 2022.

Warumi katika imani yao ya kuabudu ‘miungu’ walikuwa na ‘mungu’ wa kila jambo au tukio. Mmoja wao alikuwa Janus (mwenye uso mbele na kisogoni. Huyu Janus ambaye Walatino walimwita Ianus, anatazama alikotoka na anakoenda. Ndio mwezi tunaoingia saa sita za usiku wa leo, ukaitwa Januari. Ni muda wa watu kutafakari walikotoka, waliyopitia, walipofanikiwa, walipoteleza na waliyojifunza. Kila analopitia mwanadamu ni somo kwake. Yafaa ajiulize, “Nimejifunza nini mwaka huu wa 2021?”

Mwaka ulipokaribishwa kwa mbwembwe na vifijo, kuna watu waliojiwekea maazimio. Badala ya kuunda maazimio mapya, ni jambo la hekima kutathmini maazimio ya awali na kwa nini hayakutumia. Kisha kuwe na mpango wa jinsi ya kuyakamilisha.

Azimio kuu kwa kila mzazi ni kupata pesa za karo ili mwanawe asome shuleni bila kufukuzwa. Hili azimio litatekelezeka tu iwapo kila mzazi atavuka mwaka akijua bado kuna majukumu yanayomsubiri Januari.

Waliofanya dhihaka kuhusu mwezi huo wanasema una zaidi ya siku 31. Yaani mahitaji ya Januari ni yale yale, lakini watu wengi huwa wamefuja pesa kwa anasa za kuukaribisha Mwaka Mpya.

Kwa hivyo, kadiri watu watakavyosherehekea, watambue kuna maisha baada ya leo.

Majukumu ya Kodi ya nyumba, karo ya shule, chakula na mahitaji mengine ya msingi bado yapi palepale.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Kupuuza Okwach ndani ya timbo ni kubagua...

Kuku maridadi wa kienyeji walimaliza kiu yake ya kusaka...

T L