• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
JUMA NAMLOLA: Wanasiasa wa Kenya waige De Klerk katika kuweka mbele maslahi ya nchi

JUMA NAMLOLA: Wanasiasa wa Kenya waige De Klerk katika kuweka mbele maslahi ya nchi

Na JUMA NAMLOLA

JUMAPILI hii Novemba 21, mwili wa Frederik Willem de Klerk utachomwa kwenye hafla ya kibinafsi nchini Afrika Kusini.

F.W de Klerk si jina linalofahamika na wengi waliozaliwa miaka ya 80.

Yeye ndiye aliyekuwa rais wa mwisho wa utawala wa makaburu ulioendeleza ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Punde tu alipochukua urais kutoka kwa Pieter Willem Botha mwaka 1989, de Klerk alianza maandalizi ya kujadiliana na wapiganiaji ukombozi.

Nelson Mandela aliyekuwa kamanda wa ‘Umkhonto we Sizwe’ (Mkuki wa Taifa) alikuwa anatumikia kifungo gerezani na chama chake cha African National Congress (ANC) kilikuwa kimepigwa marufuku.

Mandela alikuwa amejiunga na vuguvugu la kutaka kukomesha ubaguzi wa rangi pamoja na Albert Luthuli, Walter Sisulu na Oliver Tambo na alikuwa anatumikia kifungo gerezani.

Alifungwa jumla ya miaka 27 na nusu kwenye magereza ya Robben Island, Pollsmoor na Victor Verster.Lakini De Klerk kwenye hutoba yake kwa Bunge la Afrika Kusini Februari 2, 1990, alitangaza kumalizwa kwa ubaguzi wa rangi, kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa na kurejeshwa kwa shughuli za vyama vya kisiasa kikiwemo cha ANC.

Na Mandela alipoachiliwa kutoka gerezani, de Klerk alishirikiana naye na kupanga uchaguzi wa urais.

Kwenye uchaguzi huo wa Mei 1994, Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini.

F.W de Klerk alilaumiwa na Wazungu wenzake kwa kuachia Weusi utawala wa nchi.

Lakini mwaka 2010 kwenye mahojiano alisema, “Kama hatungebadilisha mambo, Afrika Kusini ingekuwa imetengwa. Watu wengi duniani walitaka kutupindua. Uchumi wetu ungevurugika na ndege za Afrika Kusini hazingeruhusiwa kutua popote ulimwenguni.”

Kubwa zaidi ni kwamba, de Klerk alirekodi video ambapo aliomba radhi kwa maovu yote ya Wazungu kwa watu weusi, ikasambazwa alipokata roho Novemba 11, akiwa na umri wa miaka 85.

  • Tags

You can share this post!

Ukosefu wa sehemu maalum za kuuzia kuku wachosha...

Isuzu EA yaongeza mkataba na gunge Eliud Kipchoge kwa miaka...

T L