• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
AFCON: Morocco kukutana ama na Misri au Ivory Coast kwenye robo-fainali baada ya kung’oa Malawi

AFCON: Morocco kukutana ama na Misri au Ivory Coast kwenye robo-fainali baada ya kung’oa Malawi

Na MASHIRIKA

MOROCCO walifuzu kwa robo-fainali za Kombe la Afrika (AFCON) mwaka huu baada ya kucharaza Malawi 2-1 mnamo Jumanne usiku katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde, Cameroon.

Gabadinho Mhango aliwaweka Malawi kifua mbele katika dakika ya saba kabla ya fowadi wa Sevilla, Youssef En-Nesyri mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Beki mzoefu wa Paris Saint-Germain (PSG) alifungia Morocco bao la pili na la ushindi katika dakika ya 70.

Morocco sasa watamenyana na mshindi wa gozi jingine la hatua ya 16-bora litakalokutanisha Ivory Coast na Misri jijini Douala.

Kabla ya kipenga cha kuashiria mwanzo wa mechi kupulizwa, mashabiki na wanasoka wa vikosi vyote viwili walidumisha kimya cha dakika moja kwa heshima ya watu wanane walioaga dunia kutokana na mkanyagano ulioshuhudiwa Januari 24, 2022 nje ya uwanja wa Olembe wakati Cameroon walipokuwa wakivaana na Comoros.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Malawi kunogesha katika hatua ya 16-bora kwenye fainali za AFCON. Atlas Lions wa Morocco sasa watakuwa na kiu ya kumaliza ukame wa miaka 45 tangu watawazwe wafalme wa bara Afrika mnamo 1976. Walifungua kampeni za Kundi C kwa kupepeta Ghana 1-0 kabla ya kulaza Comoros 2-0 na kusajili sare ya 2-2 dhidi ya Gabon.

Morocco wamekuwa wakitegemea zaidi maarifa ya Romain Saiss (Wolves), Achraf Hakimi (Ufaransa), Abdessamad Ezzalzouli (Barcelona) pamoja na nyota Yassine Bounou, Munir El Haddadi na En-Nesyri.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Tabitha Karanja ajiunga na UDA

Serikali yataja mkakati wake kuwasaidia waathiriwa wa baa...

T L