• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
Arsenal waafikiana na Man-City kuhusu uhamisho wa Oleksandr Zinchenko hadi ugani Emirates

Arsenal waafikiana na Man-City kuhusu uhamisho wa Oleksandr Zinchenko hadi ugani Emirates

Na MASHIRIKA

ARSENAL wameafikiana na Manchester City kuhusu uhamisho wa nyota Oleksandr Zinchenko, hadi uwanjani Emirates kwa Sh4.2 bilioni.

Zinchenko ambaye kwa kawaida ni kiungo, aliwajibishwa pakubwa na Man-City kama beki wa kushoto mnamo 2021-22 na kwa sasa ni sehemu ya kikosi kinachofuliwa na kocha Pep Guardiola nchini Amerika kwa ajili ya kampeni za muhula ujao wa 2022-23.

Zinchenko ambaye ni raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kurejea Uingereza wiki hii kukamilisha uhamisho wake hadi Arsenal.

Zinchenko alikuwa miongoni mwa wanasoka wa kwanza kusajiliwa na Guardiola kambini mwa Man-City mnamo 2016.

Tangu wakati huo, amesaidia miamba hao kunyanyua Kombe la FA, ubingwa wa League Cup mara nne na mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Man-City wamemwajibisha mara 128 katika mashindano yote.

Zinchenko atakuwa mchezaji wa pili kuondoka Man-City na kujiunga na Arsenal muhula huu baada ya mshambuliaji Gabriel Jesus kutua uwanjani Emirates mwanzoni mwa Julai 2022 kwa Sh6.3 bilioni.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Red Devils wamnyaka Martinez wa Ajax

Zlatan Ibrahimovic atia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja...

T L