• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 11:19 AM
Bazara la Mawaziri launga azma ya Kenya kuandaa AFCON 2027

Bazara la Mawaziri launga azma ya Kenya kuandaa AFCON 2027

NA JOHN ASHIHUNDU

BARAZA la Mawaziri limeidhinisha pendekezo la Kenya pamoja na mataifa mengine jirani kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) za 2027.

Hii ni baada ya Waziri wa Biashara, Moses Kuria kufichua kwamba Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, DRC, Ethiopia na Sudan Kusini zitashirikiana kuwania uandalizi wa Afcon za 2027.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, bara hilo chini ya uongozi wa Rais William Ruto lilisema iwapo Kenya itapewa fursa hiyo, timu ya taifa Harambee Stars itatimiza ndoto ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2030.

Kadhalika, baraza hilo la mawaziri lilizungumzia suala ka kuimarisha vipaji kuanzia mashinani kama mojawapo wa njia za kuimarisha kandanda nchini.

“Serikali itafanya jitihada kuhakikisha timu ya Harambee Stars imefufuliwa pamoja na ile ya akina dada – Harambee Starlets. Kama mojawapo wa njia za kusaidia Harambee Stars kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2030, Serikali imeidhinisha mpango wa Kenya kuandaa fainali za AFCON za 2027, pamoja na mataifa mengine ya Afrika Mashariki. Uandalizi wa pamoja utakubaliwa kwa haraka na waandalizi wa michuano hiyo, kwa sababu kutakuwa na viwanja vya kutosha,” taarifa hiyo ilisema.

Kenya ilipokonywa uandalizi wa AFCON za 1996, baada ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF) kudai kwamba haikuwa na viwanja vya kutosha kufikia muda uliowekwa.

Baadaye, mnamo 2018 Kenya ilinyimwa fursa ya kuandaa fainali za Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) yanayojumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

You can share this post!

Sakaja aahidi kuboresha hospitali ya Mama Lucy

Kamishna Wanderi asema kuondolewa kwao hakutaisaidia IEBC...

T L