• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
Kenya kuandaa handiboli ya Zone 5 ya U18 na U20 Oktoba

Kenya kuandaa handiboli ya Zone 5 ya U18 na U20 Oktoba

Na AGNES MAKHANDIA

KENYA itakuwa mwenyeji wa mashindano ya chipukizi ya handiboli ya Zoni ya Tano ya Shirikisho la Kimataifa la Handiboli (IHF Trophy Africa Zone Five) mjini Nairobi mjini Nairobi mnamo Oktoba 24-30.

Uwanja wa kitaifa wa Nyayo utaandaa mashindano ya wavulana walio chini ya umri wa miaka 18 nao Ulinzi Sports Complex Lang’ata utatumika kwa wanaume wasiozidi umri wa miaka 20. Mataifa yatakayoshiriki ni Ethiopia, Uganda, Somalia, Burundi, Sudan, Tanzania, Eritrea, Djibouti na wenyeji Kenya.

Timu zitakazomaliza Zoni ya Tano katika nafasi mbili za kwanza katika vitengo hivyo viwili zitajikatia tiketi ya kuwakilisha zoni hiyo kwenye mashindano ya Bara Afrika yatakayotumiwa kuchagua timu itakayoshiriki Kombe la Dunia mnamo Desemba 12-18.

Kenya ni mabingwa watetezi katika kitengo cha U20 baada ya kulemea Ethiopia 22-17 nchini Uganda mwaka 2018. Wakenya walikamata nafasi ya nne katika U18 nyuma ya Ethiopia, Uganda na washindi Rwanda.

Mratibu wa mashindano wa Shirikisho la Handiboli Kenya, Charles Omondi alisema Alhamisi kuwa mipango imeshika kasi kuandaa mashindano ya kufana.

“Vikosi vya taifa viko tayari na timu zitaanza mazoezi juma lijalo. Najua muda ni mchache, lakini kwa bahati nzuri wachezaji wote wa U18 wanatoka katika shule za upili ambazo zimekamilisha mashindano ya kitaifa na Afrika Mashariki majuzi na ninaamini benchi la kiufundi halitakuwa na kazi kubwa kutafuta wachezaji isipokuwa kuhakikisha kuna mshikamano mzuri,” alisema Omondi.

Aliongeza, “Pia, tuko salama katika U20 kwa sababu tuna wachezaji walio shuleni na baadhi kutoka klabu wanaoshiriki kwenye Ligi ya Kitaifa na tuna uwezo wa kutosha kutawala vitengo vyote na kuingia mashindano ya bara. Tunasubiri kwa hamu kubwa kuandaa mashindano kwa sababu wachezaji wetu watapata fursa ya kupimana ubabe na marika zao.”

Mara ya mwisho Kenya iliandaa mashindano haya ni mwaka 2012.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Fuliza: Ruto sasa aokoa mahasla riba ikipungua

GWIJI WA WIKI: Kelvin Nyakundi

T L