• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Kimeumana nyumbani kwa Neymar, mpenziwe aliyejifungua juzi akimtema kwa tabia za ufisi

Kimeumana nyumbani kwa Neymar, mpenziwe aliyejifungua juzi akimtema kwa tabia za ufisi

NA CHRIS ADUNGO

SUPASTAA wa Brazil, Neymar Jr, ametemwa na demu wake Bruna Biancardi siku chache baada ya kufichuka kuwa fowadi huyo anayesakatia Al Hilal ya Saudi Arabia aliagiza kahaba amtumie picha za uchi.

Mwanamitindo Aline Farias, ambaye hunadi picha na video za uchi kwenye jukwaa la OnlyFans, aliweka peupe arafa anazodai kutumiwa na Neymar akimsihi ampe “burudani ya macho” kabla “mechi ya siri”.

Hata hivyo, sogora huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) amekanusha vikali madai hayo kwenye Instagram na kusisitiza jumbe hizo ni za zamani sana.

“Onyesha tarehe pia…Hizo ni arafa za miaka mingi iliyopita,” akaandika Neymar.

Lakini saa chache tu tangu ufichuzi huo, Bruna alichapisha ujumbe kwamba ametemana na Neymar.

Haya yanajiri wiki chache baada ya wawili hao kujaliwa binti Mavie.

“Hili ni suala la faragha. Lakini …vyema niwaambie kuwa siko tena kwenye uhusiano. Hata hivyo, mimi na Neymar ni wazazi wa Mavie na hicho ndicho cha pekee kinachotuweka pamoja. Natumai mtaelewa,” Bruna aliandika kwenye mitandao ya kijamii.

Kauli ya Bruna inachochewa na jumbe ambazo Neymar na Aline walibadilishana kwa njia ya simu ambapo sogora huyo aliuliza: “Je, kuna picha za uchi? Ziko wapi? Nataka kuona.”

Aline alimjibu kwa kuandika: “Nakutumia lakini uniambie utakachofikiria baada ya kuziona, huh.”

Baadaye, Neymar alilalamika kuwa hakuweza kupata picha hizo za kuvutia na Aline akajibu: “Lazima ujisajili mpenzi. Kunazo picha nyingi nzuri sana hapo chini. Naingia sasa kulala, jihadhari mfalme wangu. Nitakufundisha jinsi ya kuingia baadaye iwapo utashindwa kabisa. Usiku mwema.”

Ni ujumbe ambao Neymar alijibu kwa emoji ya kuashiria moto. Mvamizi huyo alianza kutoka kimapenzi na Bruna mnamo 2021. Hata hivyo, walitengana kwa mwaka mmoja baadaye kabla ya kurudiana Januari 2022.

Pindi baada ya hapo, Bruna alitangaza kuwa alikuwa mjamzito na akasema “alihisi maisha yao yalikuwa yamekamilika baada ya mtoto Mavie kuzaliwa.”

Dalili za Bruna kutemana na Neymar zilianza kuwa wazi tangu Juni baada ya sogora huyo kunaswa na kamera akisisimuana kimapenzi na wanawake wawili demu wake akiwa mjamzito.

Aliwahi pia kupapurwa peupe na kisura mmoja aliyekataa mistari yake mapenzi walipokutana kwenye hafla moja ya usiku iliyohudhuriwa na wageni 35 katika mkahawa wa Mangaritiba jijini Rio de Janeiro, Brazil, mnamo Septemba.

Neymar ana mtoto wa kiume anayeitwa Davi Lucca, 11, kutokana na uhusiano wake wa awali na kidosho Carolina Dantas aliyeanza kumfungulia mzinga wa asali akiwa na umri wa miaka 19.

Hapo awali, nyota huyo alichumbiana pia na mwigizaji maarufu wa Brazil, Bruna Marquezine, kwa miaka sita kabla ya kutemana rasmi 2018.

  • Tags

You can share this post!

Kizaazaa babu aliyeenda kununua mahaba kugundua mtumbuizaji...

Sababu ya waumini wa Akorino kuomba ‘mvua ya moto’...

T L