• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 12:35 PM
Kocha Ralf Rangnick aanza kazi ya ukocha kambini mwa Austria kwa ushindi dhidi ya Croatia

Kocha Ralf Rangnick aanza kazi ya ukocha kambini mwa Austria kwa ushindi dhidi ya Croatia

Na MASHIRIKA

KOCHA Ralf Rangnick alianza kazi kambini mwa Austria kwa kuongoza kikosi chake kupepeta Croatia 3-0 katika gozi la Uefa Nations League mnamo Ijumaa usiku.

Mkufunzi huyo raia wa Ujerumani alikuwa na msimu mgumu kambini mwa Man-United mnamo 2021-22 huku miamba hao wa zamani wakishindwa kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Hata hivyo alifungua kazi kambini mwa Austria kwa matao ya juu huku akizamisha wanafainali wa Kombe la Dunia mnamo 2018 kupitia mabao ya Marko Arnautovic, Michael Gregoritsch na Marcel Sabitzer.

Fowadi wa zamani wa West Ham United, Arnautovic ambaye kwa sasa anachezea Bologna ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) alifunga bao la kwanza la Austria chini ya Rangnick kupitia kwa kombora zito kutoka hatua ya 20 kunako dakika ya 41.

Baada ya kuzidiwa ujanja katika takriban kila idara, Croatia walimleta uwanjani kiungo mzoefu Luka Modric aliyesaidia Real Madrid kunyanyua taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2021-22.

Hata hivyo, mchango wa sogoa huyo mbunifu haukuhisika pakubwa uwanjani huku Rangnick akitamba siku chache baada ya kukataa ofa ya kuwa mshauri wa benchi ya kiufundi kambini mwa Man-United.

Kubwa zaidi katika maazimio ya Rangnick ni kuongoza ufufuo wa makali ya Austria waliodenguliwa na Wales kwenye nusu-fainali ya mchujo wa kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

Ingawa Rangnick, 63, anajivunia tajriba ya kudhibiti mikoba ya klabu 11 tofauti, hii ni mara yake ya kwanza kunoa timu ya taifa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wimbi la uhalifu Pwani

DOUGLAS MUTUA: EAC ibuni jopo la viongozi wasifika kutatua...

T L