• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
KOMBE LA DUNIA: Morocco yaandikisha historia kwa kutinga nusu-fainali

KOMBE LA DUNIA: Morocco yaandikisha historia kwa kutinga nusu-fainali

NA CHARLES WASONGA

BAO la Youssef En-Nesyri alilopachika kimiani kwa kichwa katika kipindi cha kwanza liliiwezesha Morocco kuandisha historia kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika nusu fainali za Kombe la Dunia.

Morocco iliinyuka Ureno bao hilo moja bila jibu katika mechi ya robo fainali iliyochezewa katika uwanja wa michezo wa Al Thumama, jijini Doha, nchini Qatar mnamo Jumamosi kuanzia saa kumi na mbili za jioni saa za Afrika Mashariki.

En-Nesyri, ambaye ni fowadi matata wa timu ya Sevilla ya Uhispania, aliwazuzua mashabiki wa Morocco kwa kufunga bao hilo kwa kichwa kunako dakika ya 42.

Bao hilo lilikuwa tosha kupeleka nyumbani timu ya Ureno chini ya unahodha wa staa wake matata Cristiano Ronaldo.

Morocco chini ya ukufunzi wa Walid Regragui sasa wanakutana na Ufaransa waliopiga Uingereza 2-1 jana Jumamosi. Mechi ya nusu fainali itapigwa Jumatano wiki ijayo.

Ushindi wa Morocco ni fahari kuu kwa bara Afrika ambalo wawakilishi wake wengi kama vile Cameroon, Senegal, Ghana na Tunisia walibanduliwa katika mechi za makundi.

Timu nyingine za Afrika ambazo zimewahi kufika robo fainali katika Kombe la Dunia ni Cameroon na Senegal.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Argentina sasa kuvaana na Croatia...

DARUBINI YA WIKI: Toleo Nambari 15

T L