• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 4:43 PM
Migogoro: Korti yasimamisha uchaguzi katika kamati ya Olimpiki kwa wenye ulemavu

Migogoro: Korti yasimamisha uchaguzi katika kamati ya Olimpiki kwa wenye ulemavu

NA RUTH AREGE

UCHAGUZI wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Olimpiki ya walemavu ulitibuka baada ya kuwepo amri ya Mahakama ya Kusuluhisha Mizozo ya Michezo nchini kupitia mwenyekiti wake John Ohaga.

Uchaguzi ulipangwa kufanyika hapo jana baada ya kikao cha kila mwaka katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

“Wajibu wa 1, 2 na 3 watazuiliwa na wanazuiliwa kuendelea na kuendesha uchaguzi wakisubiri kusikilizwa na kuafikiwa kwa maombi haya baina ya pande zote. Kesi hiyo hiyo itasikizwa tena tarehe 18 Oktoba 2022 saa 8:00 mchana,” uamuzi huo wa Ohaga ulisema.

Rais wa Kamati hiyo Agnes Oluoch amesema kuwa, Korti kusimamisha uchaguzi huo ambao hufanyika kila baada ya miaka minne ulikuja ghafla.

“Tulipanga kufanya uchaguzi lakini tukazuiwa na korti. Jambo kama hili liliwahi kufanyika mwaka 2014 na si jambo geni kwetu. Sisi tutafuata uamuzi wa korti na tunasubiri kwenda siku ya Jumanne kusikiza kesi hiyo,” alisema Aluoch.

Aidha anasema uamuzi huo wa korti utaathiri pakubwa timu ambayo inajiandaa kwa mashindano ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024.

“Tunatumia muda mwingi kuenda kortini badala ya kufanya mazoezi. Maandalizi yoyote hayawezi fanyika ikiwa tuna kesi kortini. Naomba wachezaji kuwa na subra tukisubiria mwelekeo. Pia tunasubiria uamuzi wa Kamati ya Kimataifa ambao pia walisema watapeana mwelekeo,” aliongezea Aluoch.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la watu wenye ulemavu wa akili Pauline Awange, amesuta kamati hiyo kwa kuwatenga.

“Kumekuwa na vuta ni kuvute tangia mwaka 2015. Uovu ambao uko kwenye kamati hii lazima ufike kikomo. Tumetengwa kwa muda mrefu, hawa wacheza wanatoka katika vitongoji duni tunataka wapewe nafasi bora,” alisema Awange.

“Kamati hii inamashirikisho manne na letu haliko. Ninafurahia kuwa korti imesimamisha uchaguzi hadi kesi hiyo ikamilike,” aliongezea Awange.

  • Tags

You can share this post!

LSK yawataka wabunge kuwakataa ‘mawaziri’ wenye...

WALIOBOBEA: Noah Wekesa ni daktari aliyejaribu siasa akavuna

T L