• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
Napoli wakung’uta AC Milan na kurukia nafasi ya pili Serie A

Napoli wakung’uta AC Milan na kurukia nafasi ya pili Serie A

Na MASHIRIKA

NAPOLI walikomesha rekodi duni ya kutoshinda mechi tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa kukomoa AC Milan 1-0 mnamo Jumapili ugani San Siro.

Ushindi huo uliwapaisha Napoli hadi nafasi ya pili jedwalini kwa alama 39 sawa na nambari tatu Milan na nne nyuma ya viongozi na mabingwa watetezi Inter Milan. Bao la pekee na la ushindi kwa upande wa Milan katika mchuano huo lilifumwa wavuni na Elif Elmas katika dakika ya tano.

Franck Kessie alidhani alikuwa amesawazishia Milan katika dakika ya 90 ila teknolojia ya VAR ikabaini kwamba alikuwa ameotea. Ushindi huo ulikuwa muhimu zaidi kwa Napoli ambao walikuwa wamepoteza mechi tatu mfululizo awali. Sasa wanaorodheshwa mbele ya Milan kutokana na wingi wa mabao.

MATOKEO YA SERIE A (Jumapili):

AC Milan 0-1 Napoli

Fiorentina 2-2 Sassuolo

Spezia 1-1 Empoli

Sampdoria 1-1 Venezia

Torino 1-0 Verona

You can share this post!

Spurs nje ya Europa Conference League baada ya kususia...

Real Madrid na Cadiz waumiza nyasi bure katika La Liga...

T L