• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:50 AM
Ndondi kutua mashinani kwa fujo hatimaye

Ndondi kutua mashinani kwa fujo hatimaye

Na CHARLES ONGADI

SHIRIKISHO la Ndondi Nchini (BFK) limeazimia kurudisha mashindano ya Ndondi Mashinani yanayolenga kuchipuza mabondia mashinani mapema baada ya kusitishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona .

Katika mahojiano na wanahabari siku ya Jumatano, mkurugenzi wa mawasiliano wa Shirikisho la Ndondi Nchini Duncun Kuria, amesema mashindano hayo yameratibiwa kurudi kwa kishindo mapema mwaka ujao.“ Mashindano haya yalinuia kuchipuza vipaji mashinani lakini yakasitishwa ghafla baada ya mlipuko wa virusi vya Corona mapema mwaka jana .,” akasema Kuria.

Aidha, Kuria amesema BFK itaendeleza mipango yao ya awali ya kutembelea klabu za mashinani na kuzipatia vifaa vya mazoezi kama njia mojawapo ya kuvumisha mchezo huu mashinani.Kulingana na Kuria ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ‘ Hit Squad ‘ mashindano ya Ndondi Mashinani yataandaliwa katika kaunti tano nchini kwa lengo la kusaka vipaji mashinani.

Wakati huo huo, Kuria amesema Shirikisho la Ndondi Nchini litaandaa mafunzo kwa marefa na makocha wa mchezo huu mapema mwaka ujao kwa lengo la kuwapasha sheria mpya ibuka kutoka kwa Shirikisho la kimataifa la Ndondi (AIBA).

“ Sheria kuhusu alama zinazotolewa bondia anapofanya makosa ulingoni zimebadilishwa kutoka alama moja hadi mbili zinazotolewa mara pigano linapomalizika, “ akasema mwamba huyu wa zamani wa timu ya taifa.Kutokana na mabadiliko hayo, shirikisho la Ndondi nchini linataka makocha na marefa kuelezwa kwa kinaga ubaga kuhusu mabadiliko hayo ili kuweza kwenda na wakati.

You can share this post!

Muturi awaita wabunge tena kujadili mswada tata wa vyama...

KK Homeboyz yagonga Tusker

T L