• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Ngetich ni nambari mbili Boston 5K, Kurgat namba tatu wanaume

Ngetich ni nambari mbili Boston 5K, Kurgat namba tatu wanaume

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Agnes Ngetich ameridhika na Sh538,400 baada ya kumaliza mbio za B.A.A. 5K nyuma ya Muethiopia Mekides Abebe mjini Boston, Amerika, Jumamosi.

Ngetich alikamilisha umbali huo wa kilomita tano kwa dakika 15:02, sekunde 0.01, huku Abebe akitwaa taji kwa 15:01 na tuzo ya Sh1.0 milioni.

Waamerika Annie Rodenfels (15:12) na Weini Kelati (15:13) walifuatana katika nafasi ya tatu na nne mtawalia kabla ya Mkenya Jesca Chelangat (15:15) kufunga mduara wa tano-bora.

Nafasi hizo huandamana na tuzo ya Sh336,500, Sh201,900 na Sh134,600, mtawalia. Kitengo cha kinadada kilivutia washiriki 4,925.

Katika kitengo cha wanaume kilichojumuisha watimkaji 3,881, Wakenya Edwin Kurgat (dakika 13:27), Alex Masai (13:27), Wesley Kiptoo (13:30) na Leonard Bett (13:30) walikamata nafasi ya tatu, nne, 10 na 11 mtawalia.

Nafasi mbili za kwanza zilinyakuliwa na Mwamerika Morgan Beadlescomb (13:25) na Ben Flanagan kutoka Canada (13:26) mtawalia.

Wakenya Peres Jepchirchir na Evans Chebet walishinda B.A.A. 5K mwaka 2022 kumaanisha kuwa Kenya imepoteza mataji yote 2023.

  • Tags

You can share this post!

Ufungaji Tata Shakahola: Watu wengine 7 wazuiliwa Malindi

Mwasisi wa Sky Digitals inayotengeneza mtambo wa Wi-Fi ya...

T L