• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Omanyala na wenzake mawindoni kutafuta tiketi ya riadha za dunia mbio za 4x100m

Omanyala na wenzake mawindoni kutafuta tiketi ya riadha za dunia mbio za 4x100m

Na AYUMBA AYODI

MSHIKILIZI wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala anatarajiwa Jumatano, Julai 12, 2023 kuongoza timu ya Kenya ya mbio za 4x100m kupokezana vijiti ya mjini Liege, Ubelgiji kutafuta kufuzu kushiriki Riadha za Dunia.

Timu ya Kenya inalenga kumaliza 4x100m chini ya sekunde 38. Kocha Stephen Mwaniki amesema kuwa watahitaji kukimbia chini ya sekunde 38 ili kuweka nafasi yao salama ya kushiriki Riadha za Dunia jijini Budapest, Hungary mnamo Agosti 19-27.

Timu hiyo ya wakimbiaji watano na kocha iliratibiwa kusafiri Julai 10 usiku ikitumia ndege ya KLM hadi jijini Brussels kabla ya kuelekea Liege, kilomita 97.2.

Omanyala, ambaye ni bingwa wa Jumuiya ya Madola na Afrika mbio za 100m, atashirikiana na Steve Onyango, Hesbon Ochieng, Boniface Mweresa na Samuel Chege katika mashindano ya Liege.

Omanyala anajivunia rekodi ya Afrika ya sekunde 9.77 kutoka mwaka 2021, lakini ameandikisha 9.84 msimu huu akishinda Kip Keino Classic Continental Tour mnamo Mei 13. Alikuwa amekimbia sekunde 9.78 (spidi ya upepo +2.3) katika riadha za Botswana Golden Grand Prix mnamo Aprili 29.

Mweresa (10.37), Onyango (10.39), Ochieng (10.47) na Chege (10.55) waliandikisha muda hiyo yao bora mwaka huu.

“Ninaamini kuwa timu yetu itapata muda unaohitajika kwa sababu iko sawa,” alisema Mwaniki.

“Mawazo yao yote yako kwa Liege na wako tayari kufanyia taifa kazi,” ameongeza Mwaniki, akisema kuwa Omanyala ni baraka kutoka kwa Mungu kwani amewapa motisha sana watimkaji atakaoshirikiana nao baada ya kufanya mazoezi pamoja ugani Kasarani.

Afisa anayehusika na mashindano wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) Paul Mutwii pia amejawa na mtumaini akisema kuwa timu hiyo itaandikisha muda mzuri ili kushiriki Riadha za Dunia kwa mara ya kwanza kabisa katika 4×100.

Kenya ingali katika nafasi ya 12 duniani katika 4x100m baada ya kuandikisha 38.26 kwenye riadha za Botswana Golden Grand Prix.

Muda huo, hata hivyo, hautarajiwi kuidhinishwa kwa sababu mmoaj wa wakimbiaji Samuel Imeta alipatikana kutumia dawa za kusisimua misuli.

Mnamo Juni 22 kwenye riadha za kitaifa, Kenya B ikiongozwa na Omanyala ilitwaa taji la 4x100m kwa sekunde 38.82, lakini muda huo ukaiweka katika nafasi ya 21.

Mutwii pia alifichua kuwa kuna mipango ya kuingiza timu ya mseto ya 4x400m katika mashindano ya True Athletes Classics mnamo Julai 29 mjini Leverkusen, Ujerumani.

Kenya inakamata nafasi ya 16 katika mbio za mseto za 4x400m baada ya kuandikisha dakika 3:14.64 kwenye riadha za kitaifa Juni 24. Mutwii alisema itategemea fedha.

Timu 16-bora katika mbio za kupokezana vijiti kufikia Julai 30 zitafuzu kushiriki Riadha za Dunia.

Timu ya Kenya Police inashikilia nafasi ya 14 duniai baada ya kutwaa taji la kitaifa kwa dakika 3:02.02 Juni 24.

AK haina mpango wa kupeleka timu ya 4x400m katika mashindano ya kufuzu nje ya Kenya.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE 

  • Tags

You can share this post!

Hatupangi ‘mapinduzi’ kwa kukusanya saini...

Uchungu wa kuona pesa za elimu ng’ambo zikizama

T L