• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Patashika Madrid! Real na Atletico kutifua kivumbi

Patashika Madrid! Real na Atletico kutifua kivumbi

MADRID, UHISPANIA

Na MASHIRIKA

UBABE wa Real Madrid chini ya kocha Carlo Ancelotti utatiwa kwenye mizani leo, watakapoalika watani wao Atletico Madrid uwanjani Santiago Bernabeu kwenye gozi moto la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Kufikia sasa, Real wanaselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 39 baada ya kushinda mechi 12, kuambulia sare tatu na kupoteza mchuano mmoja kati ya 16 iliyopita.Ni pengo la pointi saba linatamalaki kati yao na mabingwa watetezi Atletico Madrid, ambao wana alama sawa na Real Sociedad ila wanawazidia kwa wingi wa mabao kwenye mduara huo wa tatu-bora.

Ushindi kwa Real utashuhudia Atletico wakizama zaidi jedwalini, iwapo Sociedad itawapiku Real Betis ugenini nayo Villarreal ishindwe kutamba dhidi ya Rayo Vallecano ugani De la Ceramica. Barcelona na alama zao 23 watakuwa na kibarua kizito cha kujinyanyua dhidi ya Osasuna ugenini, siku tatu baada ya kuaga mapema kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Mabingwa hao mara 34 wa La Liga watajibwaga ulingoni wakiwa na kiu ya kuendeleza rekodi nzuri ya kushinda mechi tisa zilizopita katika mapambano yote. Walicharaza Sociedad 2-0 ligini wikendi iliyopita, kabla ya kusajili ushindi sawa na huo dhidi ya Inter kwenye UEFA mnamo Jumanne.

Wapinzani wao Atletico watakuwa na ulazima wa kuangusha Real ili kuweka hai matumaini ya kuhifadhi taji la La Liga msimu huu. Hata hivyo, mtihani huo utakuwa mgumu ikizingatiwa wamekuwa wakisuasua msimu huu.

Waliduwazwa 2-1 na Mallorca wikendi iliyopita ligini, kabla kutandika FC Porto ya Ureno 3-1 ugenini na kutinga raundi ya 16-bora ya UEFA.Chini ya mkufunzi wao Diego Simeone, Atleti wamepoteza alama muhimu katika mechi saba kati ya 15 zilizopita.

Atletico hawajawahi kupepeta Real ligini tangu 2015-16, walipovuna ushindi wa 1-0 ugani Bernabeu..Mechi tano kati ya nane zilizopita kati ya miamba hawa zilikamilika kwa sare, ikiwemo ya 1-1 walipokutana mara ya mwisho ugani Wanda Metropolitano kwa Atletico mwezi Machi mwaka huu.

Ingawa hivyo, ni miongoni mwa vikosi vinavyojivunia idadi kubwa zaidi ya mabao ligini baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 27. Ni Real pekee ambao wamefunga mabao magoli 37 ndio wanawazidi.Atletico hawajapepeta Real ligini tangu 2015-16 waliposajili ushindi wa 1-0 ugani Bernabeu.

Mechi tano kati ya nane zilizopita kati ya miamba hawa zilikamilika kwa sare, ikiwemo ya 1-1 mara ya mwisho ugani Wanda Metropolitano mwezi Machi mwaka huu.Huku Atletico wakitarajiwa kukosa huduma za Karim Benzema, Gareth Bale na Dani Ceballos, Atletico nao watakuwa bila maarifa ya Luis Suarez, Kieran Trippier, Stefan Savic.

You can share this post!

Hatimaye Nzoia waonja raha ya ushindi Ligi Kuu

Fainali ya Jamal Boxing yasisimua Kisumu

T L