• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 6:50 AM
Qatar kupata faida ya Sh1.1 trilioni kwa uandalizi wa Kombe la Dunia

Qatar kupata faida ya Sh1.1 trilioni kwa uandalizi wa Kombe la Dunia

MASHIRIKA Na JOHN ASHIHUNDU

TAIFA la Qatar linatarajia kupata faida ya Sh1.1 trilioni mara tu mashindano ya Kombe la Dunia yatamalizika nchini humo.

Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na kampuni ya Kamco ya Kuwait ambayo imetoa ripoti hiyo baada ya watalii wengi kuingia Qatar kwa ajili ya mechi hizo za Kombe la Dunia.

Qatar imetumia pesa nyingi kupanua miradi yake ya uchukuzi tangu 2010 hadi sasa kwa ajili ya kufanikisha maandalizi hayo ya Kombe la Dunia.

Kulingana na utafiti wa Kamco, mradi mkubwa zaidi ni ujenzi wa Lusail City ambao uligharimu Sh5.53 trilioni. Uwanja huo unaopatikana umbali wa kilomita 23 kutoka jijini Doha ndio mkubwa zaidi na una uwezo wa kubeba mashabiki 88,966.

Kadhalika, serikali ya Qatar ilitumia Sh4.43 trillioni kugharimia ujenzi wa Doha Metro sehemu ambayo imekuwa kivutio cha wageni wengi walio nchini humo wakati huu wa Kombe la Dunia, mbali na upanuzi wa uwanja wa ndege ambao uligharimu Sh1.9 trilioni.

Viwanja vingine vipya sita – Al Thumama, Al Janoub, Education City, Ahmad bin Ali, Al Bayt na Stadium 974 – vilijengwa kuongezea kwa uga wa Khalifa International Stadium ambao ulifanyiwa ukarabati.

Uwanja wa Al Bayt Stadium wenye kubeba idadi ya watu 60,000 utachezewa mechi ya nusu-fainali. Unapatikana umbali wa kilomita 35 kaskazini mwa jiji kuu la Doha. Mechi ya fainali itagaragazwa katika uga wa Lusail.

Zaidi ya wageni 1 milioni waliingia nchini Qatar kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazomaliza Jumapili, idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka, hii ni kulingana na taarifa ya FIFA.

  • Tags

You can share this post!

‘Morocco ina uwezo wa kutwaa Kombe la Dunia’

TAHARIRI: Naam, sekta ya viwanda ipewe uzito

T L