• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
Serikali yamtuza Faith Kipyegon Sh5 milioni na nyumba ya Sh6 milioni

Serikali yamtuza Faith Kipyegon Sh5 milioni na nyumba ya Sh6 milioni

NA MWANDISHI WETU

MWANARIADHA Faith Kipyegon amekaribishwa kwa njia ya kipekee baada ya kuvunja Rekodi ya Dunia katika mashindano ya mbio za mita 5000 jijini Paris, Ufaransa mnamo Juni 9, 2023.

Serikali imemtuza Sh5 milioni na nyumba ya thamani ya Sh6 milioni jijini Nairobi.

“Ninapongeza serikali kwa kuhakikisha tunapokelewa vizuri,” amesema Kipyegon leo Jumanne katika Ikulu ya Nairobi.

Akiwa na bintiye, mumewe na wazazi wake kwenye sherehe fupi katika Ikulu, Kipyegon amesema azma yake ya kumnunulia babake gari itatimia baasa ya kuandikisha rekodi ya dunia.

Nyota huyo wa mbio za mita 1,500, alimiminiwa sifa tele baada ya kufuta rekodi ya dunia ya mbio za mita 5000 kwenye riadha za Diamond League jijini Paris, Ufaransa, Juni 9, 2023.

Ilikuwa chini ya wiki moja baada ya Kipyegon kuweka rekodi ya dunia ya mbio za mita 1,500 ya muda wa dakika 3:49.11 kwenye Florence/Roma Diamond League mnamo Juni 2 baada ya kufuta ya Muethiopia Genzebe Dibaba ya 3:50.07 iliyokuwa imara tangu 2015.

Mnamo Juni 9, Kipyegon, ambaye mara ya mwisho alikuwa ameshiriki 5,000m ni mwaka 2015, alinyakua taji la Paris Diamond League la umbali huo kwa dakika 14:05.20 akivunja rekodi ya Letesenbet Gidey ya 14:06.62. Muethiopia Gidey aliweka rekodi mjini Valencia, Uhispania mwaka 2020.

Naye bingwa wa Afrika wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala amepokea zawadi ya Sh2 milioni kutoka kwa serikali ya Kenya.

Japo mapokezi katika ikulu yalikuwa ya Kipyegon na Omanyala, wanariadha wengine ambao Rais amewatunuka sifa kwa kuwataja majina ni Emmanuel Wanyonyi na Mary Moraa.

  • Tags

You can share this post!

Ajabu maiti ikifufuka Ecuador

Barobaro ajitokeza akidai yeye ni mtoto wa KRG the Don

T L