• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Soka: Green Commandos waapa kurejesha heshima yao

Soka: Green Commandos waapa kurejesha heshima yao

NA TITUS OMINDE

KIVUMBI kinatarajiwa katika michuano ya shule za upili kaunti ya Kakamega hapo kesho Ijumaa wakati michuano hiyo itaanza rasmi katika uga wa shule ya kitaifa ya Kakamega School.

Miamba wa soka wa awali Kakamega School wametilia mkazo kwamba msimu huu watarejeshea shule yao heshima ya awali wakilenga kufika fainali ya kitaifa.

Kocha wa timu hiyo, Felix Lihanda, amesema amerekebisha makosa ambayo yamekuwa yakiponza timu hiyo ambapo vijana wake wamejitolea mhanga kutwaa taji hilo.

Mwaka 2022, Kakamega walitolewa na Mwitoti kwa magoli 2-1 kwenye fainali ya kaunti.

“Hatuelewi ni vipi tulishindwa na Mwitoti mwaka 2022 lakini mwaka huu 2023 hatuna nafasi ya kupoteza. Tunalenga fainali ya kitaifa,” akasema Bw Lihanda.

Bw Lihanda amesema ni sharti watandike wapinzani wote ili kusafisha njia yao ya kufuzu kwa michuano ya kitaifa.

Kwenye raga ya wachezaji saba kila upande, mabingwa wa kitaifa Koyonzo wanajigamba kuwa watatumia kila mbinu kutetea taji hilo.

Koyonzo wametoa tahadhari kwa wapinzani wao Kakamega wakisema kuwa watawanyoa bila maji jinsi walivyofanya mwaka 2022.

“Mwaka huu wembe ni mkali kuliko mwaka 2022 ikizingatiwa kwamba vijana wako na mori isiyo na kifani. Hatutaacha kizingiti chochote,” alisema kocha wa Koyonzo Elly Okwemba.

Soka ya wavulana imegawanywa katika makundi manne sawia na wasichana.

Raga nayo imegawanywa katika makundi saba.

Kundi A la soka ya wasichana linahusisha St Joseph Mumias, Mwira, Ekatsombero na Kimangeti.

Kundi A la wavulana kuna Kakamega, Shianderema, Murkusi na Munyuki.

  • Tags

You can share this post!

Utamkumbuka Samidoh na nini akistaafu?

Kero ya kukosa matawi ya benki visiwani

T L