• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Ujerumani yazamisha Israel na kuendeleza rekodi ya kutopigwa katika mechi nane mfululizo

Ujerumani yazamisha Israel na kuendeleza rekodi ya kutopigwa katika mechi nane mfululizo

Na MASHIRIKA

MAFOWADI wa Chelsea, Kai Havertz na Timo Werner walifunga bao kila mmoja na kusaidia Ujerumani kupepeta Israel 2-0 katika mchuano wa kupimana nguvu mnamo Jumamosi usiku.

Mechi hiyo ilikuwa ya nane mfululizo kwa mabingwa hao wa dunia 2014 kusajili chini ya aliyekuwa mkufunzi wa Bayern Munich, Hansi Flick aliyemrithi Joachim Loew mnamo Julai 2021.

Havertz alifungulia Ujerumani ukurasa wa mabao katika dakika ya 36 kabla ya Werner kupachika la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Goli la Havertz lilikuwa lake la 14 katika kiwango cha klabu na timu ya taifa.

Thomas Muller wa Ujerumani alipoteza nafasi kadhaa za wazi ikiwemo penalti iliyogonga mhimili wa goli la Israel ambao pia walipoteza penalti kupitia kwa Yonatan Cohen katika dakika ya 94.

Ujerumani kwa sasa wameshinda mechi zao zote tangu kipute cha Euro 2020 kikamilike. Havertz angalifunga mabao zaidi ila akazidiwa ujanja na kipa wa Israel, Ofir Marciano. Ujerumani kwa sasa wanajiandaa kuvaana na Uholanzi katika mchuano mwingine wa kirafiki jijini Amsterdam mnamo Machi 29, 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Obiri mawindoni Istanbul Half Marathon, Kwemoi akivumisha...

Ubelgiji na Jamhuri ya Ireland nguvu sawa kirafiki

T L