• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
Youssoufa Moukoko aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao kwenye Bundesliga

Youssoufa Moukoko aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao kwenye Bundesliga

Na MASHIRIKA

TINEJA wa Borussia Dortmund, Youssoufa Moukoko, aliweka rekodi mpya ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) baada ya kucheka na nyavu mara mbili na kusaidia waajiri wake kupepeta Bochum 3-0 mnamo Jumamosi ugani Signal Iduna Park.

Bao la kwanza la Moukoko lilimfanya kuwa mchezaji mchanga zaidi, akiwa na umri wa miaka 17 na siku 350, kuwahi kufikisha mabao 10 kwenye soka ya Bundesliga.

Giovanni Reyna alifunga mkwaju wa penalti baada ya Donyell Malen kuchezewa visivyo sekunde chache baada bao la Philipp Hofmann wa Bochum kukataliwa.

Mabao yote matatu ya Dortmund yalitokana na makombora matatu ya kwanza yaliyoelekeza langoni mwa Bochum.

Mabao 12 kati ya 23 ambayo Dortmund wamefunga msimu huu yamepachikwa wavuni na matineja, yakiwemo yote matatu katika pambano lililowakutanisha na Bochum.

Ushindi huo wa Dortmund uliwapaisha hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la EPL kwa alama 25, tatu nyuma ya viongozi na mabingwa watetezi Bayern Munich waliokomoa Hertha Berlin 3-2. Bochum ambao sasa wamefungwa mabao 35 wanashikilia nafasi ya 17 kwa alama saba, moja mbele ya Schalke wanaovuta mkia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Liverpool wapewa tena Real Madrid huku Bayern Munich...

Precision Air: Mvuvi jasiri aliyekuwa mstari wa mbele...

T L