• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 11:13 AM
Gachagua asimulia jinsi Ruto alivyopata umaarufu katika eneo la Mlima Kenya

Gachagua asimulia jinsi Ruto alivyopata umaarufu katika eneo la Mlima Kenya

NA SAMMY WAWERU

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amewasuta wakosoaji wa muungano wa Kenya Kwanza, akiwataja kama ‘manabii wa uongo’.

Bw Gachagua amesema Jumapili, wapinzani wa mrengo huo tawala walitumika kama makuhani kueneza jumbe za chuki kutenganisha jamii za kutoka maeneo ya Mlima Kenya na Bonde la Ufa.

Akizungumza katika Kaunti ya Uasin Gishu, Gachagua alisema ushindi wa Dkt William Ruto naye kama Rais na Naibu Rais mtawalia kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, uliashiria wenyeji wa eneo la Kati hawashawishiwi na mawimbi ya wanasiasa aliowataja “wajibu wao ulikuwa kueneza uvumi potovu”.

“Wengine walieneza uvumi eti sisi watu wa Mlima Kenya tunadanganya Ruto. Walisema tutafuata msimamo wa Uhuru Kenyatta… Tukasema sisi ni watoto wa MauMau, tukikuahidi kitu lazima tuafikie,” Bw Gachagua akaelezea.

Alisema ushindi wa Rais Ruto ulitokana na imani ambayo jamii ya Mlima Kenya inayo kwake kukomboa uchumi wa taifa.

Naibu wa rais alisema hayo katika hafla ya maombi iliyoandaliwa Shule ya Msingi ya Koilel, Eldoret kuridhia ushindi wa Kenya Kwanza Agosti 9, 2022.

“Yeye ndiye alikuwa kiongozi wetu kuwania wadhifa wa urais, hivyo basi kuanzia leo ningependa mumtambue kama William Samoei Kamau Ruto,” akasema, jina la lakabu lililozua ucheshi miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.

Kwenye uchaguzi mkuu, Dkt Ruto alimenyana na kiongozi wa ODM aliyewania urais kupitia tikiti ya Azimio la moja One Kenya Alliance.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliunga mkono kuchaguliwa kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani.

  • Tags

You can share this post!

Uchaguzi wa Agosti 9 ulilenga kutimua waenezaji wa chuki za...

Harry Kane aongoza Spurs kucharaza Brighton katika mchuano...

T L