• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Ida aahidi kuinua maisha ya wanawake vijijini Raila akiwa rais

Ida aahidi kuinua maisha ya wanawake vijijini Raila akiwa rais

NA STANLEY NGOTHO

MKEWE kinara wa ODM Raila Odinga, Ida, ameahidi kuboresha elimu na kuinua maisha ya wanawake wa vijijini iwapo muungano wa Azimio la Umoja utashinda Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Bi Odinga alisema kuwa idadi kubwa ya wanawake wamekumbatia kilimo na biashara na wanahitaji kuwa na elimu ili kufanikiwa.

Alisema serikali ya Azimio itafanya elimu kuwa bure kuanzia shule za msingi hadi Chuo Kikuu kuwezesha kila Mkenya kupata fursa ya kusoma.

Bi Odinga alimpigia debe Raila huku akisema kuwa ataleta usawa kwa wote bila kujali kabila wala tabaka.

Alikuwa ameandamana na Gavana Joseph Ole Lenku ambapo alihutubu katika eneo la Kimana, Kajiado Kusini. Huko, alizindua Vuguvugu la Wanawake wa Azimio tawi la Kaunti ya Kajiado.

Bi Odinga na Gavana Lenku, waliwataka wakazi kutohudhuria mikutano ya kisiasa ya wanasiasa ambao hawaungi mkono.

“Ni haki yako kuunga mkono mwanasiasa yeyote unayemtaka. Ikiwa humtaki mwanasiasa fulani, hakuna haja ya kwenda kwenye mkutano wake. Tuishi pamoja kwa amani bila kuzua vurugu kwa sababu ya uchaguzi,” akasema Bi Odinga.

You can share this post!

Khaniri awarai Waluhya wamuunge mkono Raila

Kwa nini Ruto aogopa Uhuru

T L