• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:20 PM
UDA bado ndio kusema Mlima Kenya – Gachagua

UDA bado ndio kusema Mlima Kenya – Gachagua

NA KENYA NEWS AGENCY

MWANIAJI mwenza wa Kenya Kwanza Rigathi Gachagua (pichani) ameshikilia kuwa muungano huo ungali na uungwaji mkubwa katika eneo la Mlima Kenya.

Aliwataka wakazi wa eneo hilo kupigia kura wawaniaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA). Bw Gachagua alidai kuwa Azimio haijapata uungwaji wowote.

Raila Odinga ‘amejificha nyuma’ ya mwaniaji mwenza wake Martha Karua kunasa kura za eneo la Mlima Kenya.

“Tuna furaha kwamba Rais Uhuru Kenyatta amekataa kuja kumpigia kampeni Bw Odinga katika eneo la Mlima Kenya. Badala yake, Bw Odinga sasa anatumia Bi Karua kupenya katika eneo hili,” akasema Bw Gachagua.

  • Tags

You can share this post!

MITAMBO: Kifaa kinachopima ubora wa maziwa na kuepusha...

Mtafaruku Sonko akipigwa breki kuwasilisha stakabadhi kwa...

T L